Tazama Picha : MAANDAMANO YA CHADEMA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Viongozi, wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Jumatano Januari 202 wamejitokeza kwa wingi kushiriki Maandamano ya Amani katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es salaam.

Januari 13, 2024 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kufanyika kwa maandamano hayo Januari 24, 2024 akisema lengo ni kupinga miswada ya sheria za uchaguzi iliyowasilishwa bungeni.

Miswada hiyo ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa yote ya mwaka 2023.

Lengo jingine la maandamano ni kuishinikiza Serikali kusikiliza maoni ya wananchi na kutaka itengeneze mpango wa dharura wa kukabiliana kwa kupanda gharama za maisha kwa Watanzania na mfumuko wa bei.

Waandamanaji wamejitokeza wakiwa wamebeba mabango na kuimba nyimbo mbalimbali huku askari polisi wakiimarisha ulinzi katika maeneo hayo.

Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekutana na wafuasi na wanachama wa Chadema na kuwapa salamu za kubariki maandamano hayo akidai ni za Rais Samia Suluhu Hassan na kuwataka wafuasi na wanachama wa Chadema waendelee kuandamana na kufikisha ujumbe wao huku akisisitiza kila mmoja anapaswa kulinda amani.

Pia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amekutana na waandamanaji hao
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akimkabidhi barua rasmi yenye ujumne wa maandamano mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post