Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BUNGE KUANDAA MARATHON KUCHANGIA UJENZI SEKONDARI YA WAVULANA

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amesema Bunge la Tanzania linatarajia kujenga Shule ya Sekondari ya wavulana kutokana na michango itakayokusanywa kupitia mbio za marathoni zinazotarajiwa kufanyika ifikapo mwezi Aprili mwaka huu. 

Hayo yameelezwa leo January 27,2024 jijini Dodoma katika tamasha la michezo na burudani la Bunge Bonanza  lililofanyika katika Viwanja vya Jamhuri, lililo andaliwa na Benki ya Azania kwa lengo la kuwaburudisha wabunge na kujenga afya baada ya kutumia muda mwingi kwenye ujenzi wa taifa.

Amesema suala hilo linapewa  uzito mkubwa kufuatia agizo la Rais Samia kuhusu kuboresha miundombinu ya elimu kwa watoto huku akiwakumbusha wadau wa michezo kujiandikisha ushiriki wa mbio hizo.

"Safari hii Bunge marathoni itakuwa tofauti kidogo, washiriki watapata nafasi kukimbia na wabunge wao,tunakusudia kukusanya fedha kuimarisha miundombiju ya shule kwa ajili ya watoto wa kiume,tulishawahi kufanya hivyo huko nyuma kwa watoto wa kike hivyo ni zamu ya watoto wa kiume, "amesema

Katika hatua nyingine Spika Tulia ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuweza kukabiliana na magongwa yasiyo ambukiza na kueleza kuwa kufanya mazoezi ni sehemu ya kuifanya jamii kuepukana na magongwa yasiokuwa yakuambukiza amabayo yamekuwa yakiupa mzigo mkubwa serikali kukabiliana nayo.

Amesema, "Suala zima la ufanyaji wa mazoezi liliwekewa mkazo na Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambapo alisisitiza umuhimu wakifanya mazoezi kwa viongozi na jamii kwa ujumla;

"Hivyo basi kutokana na wito huo wa kujitoa na kufanya mazoezi Sisi kama viongozi wenu tumeona tuonyeshe kwa vitendo ili jamii yetu nayoifuate, " amesema 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bunge Bonanza Festo Sanga amesema bonanza hilo ni la Kwanza kwa mwaka 2024, kati ya Matatu yatakayofanyika mwaka huu, na kwamba litafuatiwa na mbio za Bunge Marathoni zinazotarajiwa kufanyika Tarehe 13 Aprili 2024.

Amesema Azania Benk wamejitoa kudhamini bonanza huku akiahidi kuwa wateja kwa shughuli mbalimali za kifedha. 

Pia amewashukuru viongozi wa Timu ya Simba na Yanga kwa kushirikiana pamoja huku wengine wakishiliki katika michezo hiyo iliyoandaliwa kwenye bonanza Hilo. 

pamoja na mambo mengine bonanza hilo limehusisha Wabunge na watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaoshabikia timu hasimu za Simba na Yanga kwa Kuhusisha. mchezo 23 ambayo yote imechezwa kwa muktadha wa timu za  Simba na Yanga. 

Katika tamasha hilo umepigwa Mchezo wa Bunge Bonanza ambapo wabunge wanaoishabikia Yanga walicheza mchezo na wabunge wanaoshabikia Simba na kwa upande wa Mpira wa Miguu Yanga wameendeleza ubabe. 

Aidha Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku bao la Yanga likifungwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said na kupelekea mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo wabunge wanaoishabikia Yanga waliwaadhibu wabunge wanaoishabikia Simba kwa  ushindi . 

Tamasha hilo limebebwa na kauli Mbiu isemayo “UTANI WETU, UMOJA WETU,” amesema Mwenyekiti huyo. 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com