Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kimetembea kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa lengo la kujifunza masula mbali mbali ya uzalishaji wa bidhaa bora zinazozalishwa na kampuni hiyo ambapo wamefurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na wawekezaji wazawa wenye tija kubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Kiongozi wa Msafara wa Viongozi wa Chuo hicho pamoja na Wanafunzi Brigedia Jenerali Baganchwera Rutambuka amesema kuwa ziara hiyo ni ya kimafunzo ambapo wamepata fursa ya kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na kiwanda hicho .
Rutambuka amesema kuwa ziara hiyo imejumuisha Wanafunzi ambao ni Maafisa wa Majeshi kutoka nchi 7 ikiwemo Zimbambwe,Rwanda,Zambia ,Misri na Algeria.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mati Super Brands David Mulokozi amesema Maafisa hao wa Jeshi na Wanafunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi walipata fursa ya kujifunza shughuli za uzalishaji na za kijamii zinazofanywa na kampuni hiyo.
"Tumewaonyesha vitu vyote hatua za uzalishaji wa bidha zetu bora kuanzia mwanzo hadi mwisho na wamefurahia kampuni ya Mati Super Brands Limited inavyofanya kazi" Anaeleza David Mulokozi Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Mati Super Brands Limited.
Social Plugin