Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, Komredi Fikile Mbalula, ambaye yuko nchini kwa ajili ya kushiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, kitakachofanyika Januari 25, 2024, nchini Tanzania. Mazungumzo ya makatibu wakuu hao wawili yamefanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), leo Jumatano, Januari 24, 2023.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akipokea zawadi ya kitabu kiitwacho "Dare Not Linger: The Presidential Years" kilichoandikwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela na Mandla Langa, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS), leo Jumatano, Januari 24, 2023.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, Komredi Fikile Mbalula, leo Jumatano, Januari 24, 2024, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo yaliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha, mkoani Pwani.
Social Plugin