Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DOLA BILIONI MBILI KUTUMIKA KUBORESHA USAFI WA MAZINGIRA ZIWA VICTORIA


KAMISHENI ya Bonde la Ziwa Victoria, inatarajia kutumia Dola za Marekani bilioni mbili kwaajili ya miradi mbalimbali ya kuweka mazingira safi ya ziwa hilo ambao utawezesha vijana wengi kupata ajira kutokana na shughuli mbalimba ambazo zitakuwa zikiendelea kufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2024 Jijini Dar es Salaam, Ofisa Miradi wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Bi.Hilda Luoga amesema wanaangalia maendeleo endelevu ya Ziwa Victoria kwa kuandaa mikakati ya mradi kwa kutatua changamoto na kukabili uchafuzi wa mazingira ya ziwa hilo kwa majitaka yanayotoka kwenye makazi ya watu na kwenye viwanda na matumizi mabaya ya ardhi.

Aidha amesema kuwa Benki kuu ya Dunia (WB) imekuwa ikifadhili Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi katika miradi ya kukabiliana na uchafuzi wa ziwa na mwaka 2020 ilifanya utafiti wakakuta kuna vyanzo vikuu vitatu kwenye ziwa hilo.

"WB ilibaini kuwa uchafuzi huo unatokana na vyanzo vikuu vitatu ambavyo ni majitaka kwenye makazi, kutoka kwenye viwanda na matumizi mabaya ya ardhi". Amesema

Kwa Upande wake Meneja wa Tafiti za mazingira akimwakilisha Mkurugenzi wa NEMC Bi.Rose Salema Mtui amesema Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na Taasisi ya Sayansi na Mazingira (CSE) ya India, wameendelea na mkutano wa wadau wa Mazingira wa ziwa Victoria kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Mashirika ya kikanda, Wizara, Mikoa na Halmasahauri kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mkakati wa usimamizi wa mazingira wa Ziwa hilo.

Programu hiyo ya Pamoja ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji ya Ziwa Victoria katika mradi huo unatarajiwa kugusa maeneo muhimu yanayochochea uchaguzi wa maji ambayo ni Homabay-Kenya, Entebbe-Uganda na Mwanza-Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com