Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akizungumza na Afisa Masoko kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Victoria John Mwakalasya alipotembelea Banda la MSCL kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Masoko kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Victoria John Mwakalasya kuhusu kazi zinazofanywa na Kampuni hiyo alipotembelea banda la MSCL kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
...............
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihezile ameielekeza Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha wanaitangaza meli ya mizigo ya MV. Umoja kwa kutumia njia mbalimbali za vyombo vya habari na maonesho mbalimbali ili kuendelea kuwajulisha wafanyabiashara wakubwa juu ya uwezekano wa kusafirisha mizigo kutoka Tanzania kwenda Uganda na Kenya kwa kuitumia meli hiyo inayofanya kazi katika Ziwa Victoria.
Mhe. Kihenzile ameyasema hayo mara baada ya kutembelea Banda la MSCL katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar hivi karibuni
Meli ya mizigo ya MV. Umoja inafanya safari zake kati ya Mwanza, Tanzania na Portbell na Jinja, Uganda pamoja na Kisumu nchini Kenya.
Social Plugin