Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche Amefungiwa Mechi nane na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kufuatia kauli zake alizozitoa kuwa Morocco ina ushawishi ndani ya CAF katika kupanga mechi pamoja na waamuzi.
Kufuatia adhabu hiyo, Kamati ya Utendaji ya TFF pia imemsimamisha kocha huyo na kumteua Hemed Morocco kuwa Kaimu Kocha akisaidiana na Juma Mgunda.
Kocha Amrouche amefungiwa ikiwa ni siku moja imesalia Stars kushuka dimbani dhidi ya Zambia kesho Januari 20,2024.
Social Plugin