Picha : JUMUIYA YA WAZAZI CCM MKOA WA SHINYANGA YAADHIMISHA MIAKA 47 YA CCM... SIAGI ASISITIZA UTAWALA BORA KWA VIONGOZI

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga imeadhimisha miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama hicho kilichoanzishwa mnamo Februari 5, 1977  kwa lengo la kuendelea kukienzi Chama cha Mapinduzi na kuimarisha jumuiya hiyo.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Januari 26, 2024 katika uwanja wa shule ya kanisa la Anglikana kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga.

Awali akizungumza na wananchi wa Chama Cha Mapinduzi na viongozi wakati wa kikao cha ndani Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi amewakumbusha wanachama na viongizi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi za kata na wilaya juu ya ya uwajibikaji katika siku adhimu ya kumbukizi ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977.
"Kiongozi ana wajibu wa kutambua majukumu yake na kuonyesha dira kwa wale anaowaongoza, kiongozi yeyote akisimama kwenye kanuni zilizowekwa na Chama Cha cha Mapinduzi kupitia Jumuiya ya wazazi wa chama hiki atakwenda vizuri, awe mbunifu kwenye uongozi, awe na imani na watu anaowaongoza, awe ni mtu asiyetawaliwa na tamaa lakini pia awe anapenda kujitolea kufanya kazi za jumuiya na chama wakati wote lakini ukishindwa kusimama kwenye majukumu na wajibu wako kama kiongozi utashindwa kuongoza vyema", amesema Siagi.

"Sisi kama chama na Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi tuna wajibu wa kupinga na kukemea vitendo vya ukatili kupitia mikutano yetu, ni lazima tukumbushane ili kuimalisha Jumuiya yetu na Chama cha Mapinduzi kwa ujumla", ameongeza Siagi.

Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga John Siagi amesihi wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu kufuatia taarifa za mlipuko wa ugonjwa huo ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

"Lakini pia tuchukuwe tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu ambao kwa sasa umeshika kasi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na mkoa wetu wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa iliyolipotiwa kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo, tujitahidi kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ili kuepukana na ugonjwa huu", amesema Siagi.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya kanisa la Anglikana diwani wa kata ya Ndala Zamda Shabani amesema serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefanya maendeleo makubwa kwenye kata ya Ndala katika sekta mbalimbali.

" Kwenye sekta ya elimu tulikuwa na changamoto ya madarasa, matundu ya vyoo lakini ndani ya miaka 3 tumepokea zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kutatua changamoto hizo, pia katika miundombinu tumeendelea kukarabati na kutengeneza ndani ya kata hii alikadharika pia upande wa afya, Watu wa Ndala tunaishukuru sana serikali kupitia Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na mbunge wetu Patrobas Katambi tuwaahidi mitano tena", amesema Diwani Zamda Shabani.

Akizungumza kwenye mkutanio wa hadhara mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Mhe. Patrobas Katambi amesema katika kipindi cha miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi mengi yametekelezwa kupitia ilani ya chama hicho ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, barabara, shule, maji na kuwaahidi wakazi wa kata ya ndala kuanza ujenzi wa barabara ya Ndala - Mwawaza kwa kiwango cha Lami.
"Tuna mengi ya kujivunia katika miaka 47 ya Chama cha Mapinduzi hapa nchini, shule zilizokuwa shikizi zimekuwa kamili ikiwemo za msingi na sekondari, na Kupitia mkutano huu niwahakikishie changamoto ya hii barabara ya Ndala hadi Mwawaza inakwenda kuisha na kubaki historia, kupitia ahadi iliyowekwa na serikali kwani tayari tumekwisha anza kupokea fedha kwaajili ya barabara hiyo", amesema Katambi.
"Katika miaka kuadhimisha miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi mengi tumetekekeza kupitia ilan ya chama chetu, ushindi upo kwetu sababu tuna kila savabu ya kushinda", ameongeza Katambi.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga John Siagi (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi wakati wa Mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Shinyanga mjini Fue Mrindoko akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara.
Katibu wa Jumuiya wazazi Mkoa wa Shinyanga Regina Ndulu akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara.

Mjumbe Kamati ya Utekelezaji Mkoa Agness Kahabi akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza wakati wa kikao cha ndani.
Mkutano wa hadhara ukiendelea.



Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushiriki kwenye mkitanio wa hadhara.


Mwenyekitri wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi mkowa wa Shinyanga John Siagi pamoja na mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi wakikabidhi mipira na jezi kwa vijana watakao shiriki mashindano ya miaka 47 ya CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post