Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA GIZ LATOA MSAADA WA VIFAA VYA TEHAMA HOSPITALI YA KOROGWE MJI

 

Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe kulia akikabidhi vifaa vya Tehama wa kwanza kushoto ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Mark Tanda akifuatiwa na Mratibu wa GIZ Apolinary Primus 


Sehemu ya Vifaa hivyo












Na Oscar Assenga, KOROGWE.

Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) limetoa msaada wa vifaa vya tehama katika Hospitali ya Mji wa Korogwe ya Manundu na kuweka miundombinu ya Intaneti,Ufugaji wa Mfumo wa kieletroniki ambao ni mfumo wa taarifa za usimamizi wa Hospitali za Serikali ya Tanzania (GoTHOMIS) pamoja na kufanya mafunzo endelevu kwa watumishi.

 Ambapo hadi sasa zaidi ya wafanyakazi 150 katika hospitali ya Korogwe tayari wamefundishwa jinsi ya kutumia mfumo wa GoTHOMIS ambapo uwekezaji wake wa awali umegharimu Milioni 200,000,000 uliofanywa na GIZ hadi sasa na msaada zaidi ya kuifundi umepangwa ili kuhakikisha lengo linafikiwa ifikapo mwaka 2025.

 Akizungumza wvakati wa makabidhiano rasmi ya vifaa vya Tehama, Kaimu Meneja wa Mradi wa Afya wa GIZ Tanzania Erick Msoffe amesema kuwa mpango huo unalenga kubadilisha taratibu za kiutawala na kiafya katika hospitali hii kwa kuondoa matumizi ya kumbukumbu za karatasi, kuboresha uhifadhi na upatikanaji wa takwimu za wagonjwa, kuongeza hospitali ufanisi na kupunguza makosa katika takwimu.

Alisema kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani ambao ni wafadhili wao lakini pia wameshirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya pamoja na  Ofisi ya Rais Tamisemi wamekuwa wadau kwa mkoa wa Tanga kwa miaka tisa kwa awamu ya miaka mitatu mitatu.

Msoffe alisema kuwa mara nying wamekuwa kwenye awamu uliyoanza mwaka 2023 na itakwenda mpaka 2026 kwa mkoa wa Tanga na wana jumla ya Hospoitali 18 wanazozisaidia lakini katika eneo la Tehama pamoja na kwamba huyko nyumba wamefanya kazi na Hospitali nne kwenye eneo hilo lakioni watawasapoto kuweka miunbdombi na kuwafanya mafunzo watumishi waweze kuutumia.

 “Kwanini tupo Korogwe kuhakikisha sisi kama wadau na Serikali ikiwemo Hospitali wanaweza kufanya juhudi za kipekee kuona ni gharama gani zinahitajika ili kuitoa Hospitali ya wilaya kutoka kwenye matumiz ya mifumo ya katarasi na kwenda katika asilimia 100 ya matumizi ya Kiletroniki”Alisema

 Alisema katika mafanikio yatakayopatikana katika hospitali ya Korogwe, yatatumiwa na serikali ya Tanzania kuongeza mageuzi haya ya kidijitali kwa hospitali nyingine chini Tanzania.

“GIZ inaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira bora ya kisera na kutoa msaada wa kitaalamu katika kuboresha huduma za afya chini Tanzania”Alisema.

Alisema maboresho hayo yanayoendelea katika mifumo ya kidigitali na hasa mfumo wa GOTHOMIS ambao ni moja ya mifano tosha ya dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kusaidia vituo vya afya kuboresha huduma za afya kupitia teknolojia ya kidijitali.

 Hatua hiyo ni moja ya mambo ya msingi ya kuongeza ufanisi Hospitali ya Mji wa Korogwe inatangaza kwa fahari uamuzi wake wa kuachana na mifumo inayotumia makaratasi kabisa. Hospitali hiyo inakumbatia manufaa ya teknolojia katika kuimarisha huduma za afya na kurahisisha shughuli mbali mbali.

 Uamuzi huo umekuja baada ya ongozi na wafanyakazi kutambua changamoto zinazoendelea kukabili mfumo wetu wa huduma za afya zikiwemo uhaba wa watumishi, kazi kubwa inayowakabili watumishi kwa kujaza karatasi nyingi, takwim duni lakini pia muda mrefu ambao wagonjwa hukaa hospitalini kupata huduma.

Kwa hiyo hospitali ya Korogwe imejitolea kutumia maendeleo ya kidijitali ili kutoa huduma ya hali ya juu kwa wateja wake. Kuachana na matumizi ya makaratasi na kuharnia mifumo ya kidigitali ni tatua muhim katika kufikia lengo hili.

 Deutsche Gesellschaft fur Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH kupitia mpango wake wa afya wa Kuboresha Huduma ya Afya Tanzania (ICP) ni mshirika wa muda mrefu na wamekuwa wakisaidia mkoa wa Tanga na haswa hospitali ya Korogwe kutekeleza afua za afya za kidijitali ambazo zinalenga kuongeza fanisi na ubora wa huduma za afya.

Awali akizungumza Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mji wa Korogwe Dkt Heri Kilwale alisema kuwa kubadilika kutoka matumizi ya karatasi na kutumia mifumo ya kidijitali itawasaidia watoa huduma za afya kuweza kupata taarifa za mgonjwa kwa wakati na salama.

Alisema pia kutapunguza muda ambao wafanyakazi hutumia kufanya kazi za kujaza makaratasi mengi na hivyo wataalamu wa afya wataelekeza zaidi muda katika kutoa huduma kwa wagonjwa na hivyo kupelekea kuongezeka kwa ubora wa huduma zinazotolewa.

Korogwe ni miongoni mwa hospitali chache ambazo zimeanza kutumia toleo jipya la GoTHOMIS na kva msaada wa mara kwa mara kutoka kwa serikali, ongozi wa hospitali na washirika wa maendeleo, inatarajiwa kuwa hospitali ya Korogwe itafanikiwa katika dhamira yake ya mabadiliko kutoka matumizi ya karatasi Kwenda katika mifumo ya huduma za kidijitali na kwamba. Serikali itapanua msaada huo kwa hospitali zingine baada ya hapo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com