MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) wanaendesha mafunzo ya masuala ya uongozi wa kijinsia ili wanajamii waweza kuenzi nguvu za pamoja, na kuhusisha wanawake katika ngazi za maamuzi ikiwa ni sehemu ya kuleta mabadiliko kwenye jamii na kuwainua kiuchumi.
Mafunzo hayo ya siku kumi kwa ajili ya masuala uongozi wa kijinsia wamewajumuisha wanawake kutoka nchi mbalimbali za afrika ikiwemo kenya, uganda, zimbabwe, rwanda, Ghana, burundi, afrika kusini na Nigeria.
Ameyasema hayo Januari 27, 2024 Jijini Dar es Salaam, Afisa wa program Mafunzo wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Anna Sangai kuwa washiriki hao wamejifunza wanajamii wanaweza kuenzi nguvu za pamoja na kuhusisha wanawake katika ngazi za maamuzi.
Pia washiriki hao walitembelea kituo cha taarifa na maarifa kipunguni lengo ni kujifunza wanawake walivyowezesha kubadilisha jamii juu ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa maswala ukeketaji, mimba za utotoni, ukatili wa vipigo na kutunza mazingira ili kuwawezesha wanawake kiuchumi.
Sangai amesema wanawake wamefundishwa jinsi ya kutengeneza mkaa mbadala ambao wanatumia kwenye matumizi yao, nakuuza ili kujipatia fedha katika kukuza uchumi wao, pia wametumia mbolea kuzalisha wadudu kupitia takataka ambao wanakuwa chakula cha kuku n.k
"Katika hayo majumuiko ya kujifunza wametumia kama fursa ya kupata taarifa ya ukeketaji, watoto kuozeshwa kwenye umri mdogo, wanaotembea na wanafunzi, vipigo ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake kwa baadhi ya ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia" amesema Anna Sangai
Social Plugin