TGNP YAFUNGUA MAFUNZO YA USHIRIKIANO KATIKA UKOMBOZI WA WANAWAKE KIMAPINDUZI NA KUONDOA DHANA YA UKOLONI

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa Asasi za Kiraia na makampuni binafsi kutoka nchi kumi barani Afrikayenye lengo la kushirikiana katika masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi ili kuondoa dhana ya ukoloni.  Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Januari 22,2024 katika ofisi za TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.

****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamefungua mafunzo ya kikanda ambayo yanahusisha washiriki kutoka nchi kumi za bara la Afrika ambao wanatoka katika Asasi za Kiraia na Mkampuni binafsi yenye lengo la kushirikiana katika masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi ili kuondoa dhana ya ukoloni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 22,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi amesema mafunzo hayo yatajikita zaidi kuonesha uongozi ambao unafuata misingi ya haki za binadamu ambao unagusa mgawanyo sawa wa rasilimali kwa makundi yote.

"Tunapozungumzia kwamba(Decolonization of Feminist Leadership) tunamaanisha kuondoa dhana ya Ukoloni katika Uongozi ambao ni uongozi wa kimapinduzi unaoangalia katika suala la haki na usawa, sisi kama wanawake tumejikita katika uongozi umbao una ubinadamu". Amesema Bi. Lilian.

Aidha Bi.Lilian ameeleza kuwa mafunzo hayo kupitia wataalamu ambao watafundisha katika mafunzo hayo watajikita hasa jinsi ya kuweka mikakati itakayogusa kutatua changamoto za kila kundi bila kumuacha mtu nyuma.

Pamoja na hayo ameipongeza taasisi ya Chuo Kikuu cha COADY INTERNAL INSTITUTE kinachopatikana Canada ambao wamekuwa wakishirikiana katika mafunzo mbalimbali ya uongozi kwa wanawake waliopo kwenye vituo vya Taarifa na Maarifa, na masuala ya maendeleo na uwezashaji wa wanawake kiuchumi.

"Katika haya mafunzo napenda kuushukuru Ubarozi wa Canada kupitia Global affairs Canada ambao wamewezesha mafunzo haya na wamekuwa wakitusaidia katika Mikakati yetu mbalimbali kwa zaidi ya miaka mitano katika mradi mkubwa unaohusu ushiriki wa wawanawake na Sauti za wanawake katika Uongozi ambao tumeutekeleza kwa zaidi ya miaka mitano sasa". Bi.Lilian amesema.

Kwa Upande wake,Afisa Programu wa Taasisi ya COADY kutoka Canada Bw.Erick Smith amesema kuwa amefurahi kushiriki katika mafunzo hayo ya kuondoa Ukoloni katika Uongozi kwa wanawake kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia TGNP ambayo yanakutanisha watu mbalimbali ambapo watatambua na kuchunguza changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa katika mfumo wa kikoloni katika ulimwengu.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Glaring Future Fondation Bi.Aisha Msantu amesema kuwa anatarajia kunufaika kutokana na mafunzo hayo ambayo yataleta mapinduzi dhidi ya dhana ya Ukoloni na kuleta matokeo chanya katika jamii kwenye suala la usawa wa Kijinsia.

Vilevile Afisa Programu na Uwezeshaji wanawake kiuchumi wa Pelum Tanzania Bi.Anna Marwa amesema anatarajia kuongeza ujuzi kupitia mafunzo hayo katika masuala ya Uongozi kwani changamoto zinazowakabili wanawake kuingia katika Uongozi Afrika kwa sehemu kubwa yanafanana.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku Kumi Januari 22-31,2024 yamehudhuriwa na zaidi ya nchi Kumi za Afrika miongoni ni Kenya, Ethiopia,Afrika Kusini, Cameroon na Canada kutoka nje ya Africa ambapo umehusisha washiriki walio hudhuria kuwakilisha serikali zao,Asasi za kiraia na binafsi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi akifungua mafunzo kwa Asasi za Kiraia na makampuni binafsi kutoka nchi kumi barani Afrikayenye lengo la kushirikiana katika masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi ili kuondoa dhana ya ukoloni.  Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Januari 22,2024 katika ofisi za TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa Asasi za Kiraia na makampuni binafsi kutoka nchi kumi barani Afrikayenye lengo la kushirikiana katika masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi ili kuondoa dhana ya ukoloni.  Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Januari 22,2024 katika ofisi za TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa Asasi za Kiraia na makampuni binafsi kutoka nchi kumi barani Afrikayenye lengo la kushirikiana katika masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi ili kuondoa dhana ya ukoloni.  Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Januari 22,2024 katika ofisi za TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa watoa mada kutoka nchini Canada akiwasilisha Mada kwenye Mafunzo kwa Asasi za Kiraia na makampuni binafsi kutoka nchi kumi barani Afrikayenye lengo la kushirikiana katika masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi ili kuondoa dhana ya ukoloni.  Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Januari 22,2024 katika ofisi za TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Bi.Lilian Liundi akipata picha ya pamoja na washiriki kutoka nchi kumi za bara la Afrika ambao wanatoka katika Asasi za Kiraia na Mkampuni binafsi wakati wa ufunguzi wa mafunzo yenye lengo la kushirikiana katika masuala ya jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi ili kuondoa dhana ya ukoloni. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Januari 22,2024 katika ofisi za TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam.

 (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO) 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post