Mkurugenzi wa TGNP Bi. Lilian Liundi akichangia jambo katika semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) ambazo zimekuwa zikifanyika kila siku ya jumatano katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam.
*************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) umetoa mapendekezo yake yenye lengo la kuhakikisha maswala ya msingi ya kijinsia yanazingatiwa katika Mchakato wa kurekebisha Sheria za uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 17,2024 katika ofisi za TGNP Mtandao Mabibo- Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TGNP Bi. Lilian Liundi amesema uchaguzi wa serikali za mitaa unapokaribia huwa wanatoa ilani yao ya wanawake ambapo hubaniisha masuala ya msingi ambayo wanahitaji kuyaona katika uchaguzi.
"Ukisoma ilani yetu, mapendekezo ya kwenye Sheria hizi ni yaleyale tuliyokuwa tunayajadili kila wakati na yako kwenye ilani yetu ambayo tuliizindua Novemba 2023, kwahiyo maoni hayo ndiyo tuliweza kupata kupitia ile miswada tulifanya uchambuzi na kuwasilisha". Amesema Bi. Lilian
Aidha Bi.Lilian ameeleza kuwa baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo wamekutana kujadili masuala muhimu ya kijinsia ambayo yanatakiwa kutiliwa uzito katika Mchakato huo wa uchaguzi.
"Kwenye Sheria ya uchaguzi wa madiwani,wabunge na Rais tumetoa pendekezo la jumla tukiangalia katika uchaguzi wa Rais hili nipendekezo letu kwamba vyama vya Siasa kama vikipendekeza mgombea wa urais kama mgombea ni mwanaume basi mgombea mwenza awe mwanamke kama mgombea ni mwanamke basi mgombea mwenza awe mwanaume ili kwa njia hiyo tutakua tumezingatia usawa wa kijinsia kwenye hili ni pendekezo letu kwenye ile miswada haipo". Ameeleza.
Amesema wameangazia katika suala la dhamana pale kwenye mchakato wa kurejesha fomu baada ya kujaza waliangalie vizuri kwani ni sababu inayochangia kuzorotesha ushiriki wa Wanawake katika uchaguzi kwa sababu ya kukosa fedha hasa kwa wanawake na walemavu ambapo kwa mapendekezo yao ni kwamba mtu akishakuwa mwanachama wa chama cha siasa iwe ndio dhamana yake.
Pamoja na hayo amesema wameona ni vyema watendaji wa tume wawe ni waajiriwa wa kudumu kwa lengo la kutunza kumbukumbu vizuri ili kuondokana na kutumia watendaji wa serikali na ulalamishi katika mchakato wa uchaguzi.
Vilevile amesema kuwa kuna baadhi ya makosa ambayo hayajabainishwa katika muswada huo wa uchaguzi kama masuala ya makosa ya ukatili wa kijinsia ambapo inapelekea kuwepo kwa ushiriki hafifu kwa wanawake katika mchakato wa uchaguzi na kusabishwa kuwepo kwa malalamiko mengi.
Bi.Lilian amesema kuwa ili kutoa wigo wa ushiriki wa wanawake na walemavu kunatakiwa kuundwa kikosi maalumu kwa ajili ya kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama katika uchaguzi ili kuondoa hali ya hofu kwa wapiga kura.
Kwa upande wake,Mdau wa semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) Bw.Nobart Dotto amesema kuwa wamejifunza na kutambua muswada unazungumzia nini ambapo wameadhimia kushirikisha. wadau wengine ikiwemo vyombo vya habari kwa lengo la kusukuma ajenda zao ili zitekelezwe na mamlaka husika.
Naye Mdau wa jinsia kutoka kituo Cha Taarifa na Maarifa Kata ya Mabibo Bi. Jamila Kisinga ameeleza kuwa wameadhimia kuishinikiza serikali isipuuzie yale mapendekezo yaliyotolewa na wanajamii na taasisi mbalimbali ambayo hayajakaa katika mlengo wa kijinsia wakati tunapoelekea katika uchaguzi.Mkurugenzi wa TGNP Bi. Lilian Liundi akichangia jambo katika semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) ambazo zimekuwa zikifanyika kila siku ya jumatano katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam
Mwezeshaji Deogratius Temba akiwasilisha mada isemayo 'Masuala ya msingi ya kijinsia kuzingatiwa katika mchakato wa kurekebisha sheria za uchaguzi' wakati wa semina za jinsia na maendeleo ambazo zimekuwa zikifanyika kila siku ya jumatano katika ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam
Mwezeshaji Deogratius Temba akiwasilisha mada isemayo 'Masuala ya msingi ya kijinsia kuzingatiwa katika mchakato wa kurekebisha sheria za uchaguzi' wakati wa semina za jinsia na maendeleo ambazo zimekuwa zikifanyika kila siku ya jumatano katika ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam
Mdau wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) akichangia jambo katika semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) ambazo zimekuwa zikifanyika kila siku ya jumatano katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam
Mdau wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) akichangia jambo katika semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) ambazo zimekuwa zikifanyika kila siku ya jumatano katika Ofisi za TGNP Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Social Plugin