Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda akizungumza katika Mkutano na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda,(hayupo pichani) wakati wa kikao na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima kilichofanyika leo Januari 30,2024 jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu ,Dodoma .
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT Mary Chatanda amefanya Kikao na Wabunge wanawake wa CCM Nchi nzima lengo Likiwa ni Kuwasihi kuendelea kufanya kazi kwa kuwatumikia wanawake na wananchi Nchini kwa kufanya Mikutano ya Hadhara ya kuisemea Miradi ya Serikali iliyofanywa na Serikali ya awamu sita chini ya uongozi wake Dkt Samia SuluhuHassan.
Akizungumza leo na Wabunge wanawake wa CCM Nchini Mwenyekiti Chatanda amesema Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi katika Mikoa yenu basi sasa niwaombe wabunge muendelea kutembelea miradi na kuisemea kwa wananchi ili wajue Serikali yao imefanya nini kwenye maeneo yenu.
Mwenyekiti Chatanda amewaomba Wabunge wanawake wa CCM Nchini kuendelea kuhamasisha wanawake kushiriki kwenye Uchaguzi na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa ambayo utaaza hivi karibuni.
"Sisi ndio Jeshi la Mama basi niwaombe wanawake wenzangu mwende kwenye Mikoa yenu fanyeni Mikutano ya Hadhara na kuhamasisha wanawake kugombea kwani wanaweza endapo mkiwahamasisha watahamasika kwa kasi"
Hata hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema nimefurahishwa sana na baadhi ya wabunge wanawake ambao wanaendelea kupambana katika kuhakikisha wanafanya Mikutano ya Hadhara na kusemea miradi iliyofanywa katika maeneo yenu hivyo niwaombe muendelee na juhudi hizohizo katika kusemea Serikali ya Rais samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti Chatanda amesema Wabunge wangu Nawapenda sana sana muendelea kupambana katika kuhakikisha wananchi na wanawake walipo katika maeneo yenu wajue nini Serikali yao inafanya katika kuwaletea Maendeleo.
Nae Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Zainab Shomari amewapongeza wabunge wanawake kwa kufanya kazi katika Mikoa yao na kuwaomba kuendelea na juhudi hizo katika kusemea miradi na kusikiliza kero za wanawake na kuweza kutatua kwa wakati.
"Sisi kama viongozi wenu tupo pamoja na nyie katika kutatua changamoto yoyote ambayo inakwamisha kazi zenu na niwaombe muendelee na juhudi hizohizo katika kutatua Migogoro na changamoto zilizopo katika maeneo yenu."
Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jokate Mwegelo amewashukuru wabunge wanawake kwa kujitoa kwa wingi kuja kusikiliza Mwenyekiti na kuwaomba yale yote ambayo Mwenyekiti kazungumza basi yafanyiwe kazi ipasavyo kwa Maslai ya Jumuiya yetu ya Wanawake.
Social Plugin