Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA WAPINGA MAANDAMANO YA CHADEMA


Na Mwandishi Wetu, Lindi

JUMUIYA ya Wafanyabishara Tanzania (JWT), imepinga uwapo wa maandamano yaliyoitishwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa sababu waathirika wakubwa wa ni wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kando ya barabara na mitaani.

Maandamano hayo yamepangwa kufanyika Jumatano ya wiki ijayo, Januari 24, 2024, kuanzia Mbezi Luis Standi ya Magufuli kuelekea hadi Ofisi za Umoja wa Mataifa mkoani Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa JWT, Hamis Livembe, akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Lindi, amewataka wanasiasa ambao wana hoja zilizotofautiana na serikali kurudi kukaa mezani ili kupata suluhu badala ya kufanya maandamano hayo.

"Sisi wafanyabishara tunapinga haya maandamano kwasababu sisi ndio waathirika wakubwa kwa kuwa yanapita sehemu zetu za biashara na wao wanapenda kupita sehemu zenye biashara na mikusanyiko ya watu wengi, zinapotokea rapsha maduka yanavunjwa, kufungwa, fujo na siku hiyo bishara zinakuwa haziwezi kufanyika kwa hiyo sisi tunapinga jambo hili," amesema Livembe.

Ametolea mfano maandamano yaliyofanyika nchini Kenya hivi karibuni na kusema walioathirika ni wafanyabishara ambao walishindwa kuendelea na kazi na wengine biashara zao ziliharibiwa.

"Hapa Tanzania nimeambiwa yanataka kuanzia Mbezi Magufuli pale tuna wafanyabishara karibu 2,000 lakini barabara walizochagua kupita kuna watu wanafanyabishara kando ya barabara, kuna mabasi, magari ya abiria, tax na ubber ambazo zinaweza kuathiriwa kama maandamano yatafanyika, hivyo tunashauri wanaioopingana na serikali watafute njia nyingine za kufanya lakini wasisumbue wafanyabishara wetu," amesisitiza Livembe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com