Msafara wa Katibu wa NEC Itikadi ,Uenezi na Mafunzo wa CCM Paul Makonda umepata ajali katika eneo la Masasi mkoani Mtwara.
Ajali hiyo iliyotokea leo Jumapili saa 9 alasiri imehusisha magari 10 yaliyokuwepo katika msafara wa muenezi Makonda uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea jijini Dar es salaam
Taarifa zilizothibitishwa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu wawili wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote.
Hata hivyo kwa upande wa hali ya kiafya ya katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Paul Makonda ipo salama.
Chanzo - Wasafitv
Social Plugin