Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato ambaye pia ni Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki
Na Mariam Kagenda _ Bukoba
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo Februali 23 2024 amefika kata ya Bakoba na kuzungumza na wananchi wa kata hiyo.
Licha ya kuzungumza na wananchi hao pia amekagua shughuli za wafanyabiashara wadogo na kupitia eneo la mradi wa TACTIC katika barabara ya Shabridin kuangalia maandalizi ya mapokezi ya mradi huo mkubwa.
Mhe. Adv. Byabato alipata fursa ya kuzungumza na wananchi wanaopatikana katika maeneo hayo na kuwaeleza juu ya miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya manispaa ya Bukoba pamoja na kuwaomba wananchi hao kuendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi waliopo kuanzia kwa wenyeviti, madiwani na yeye mbunge ili mambo mazuri yaendelee kutekelezwa kama ilivyoahidiwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.
Kwa upande wake diwani wa kata Bakoba Mhe Shabani Rashidi wakati akimkaribisha Mhe Mbunge baada ya kufika katika kata hiyo amesema kuwa wanabakoba wanajivunia uongozi wa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mbunge wa jimbo la Bukoba Mhe Stephen Byabato kwani kila sehemu kuna mradi wa maendeleo unaoendelea hivyo wanaamini miradi vipolo ikikamilika watakuwa hawana deni kwa wananchi.
Aidha Mhe. Shabani amesema kuwa wanaendelea kushirikiana kushirikiana na wananchi katika maeneo tofauti tofauti katika kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali za kutatua kero za wananchi.
Mhe.Adv Byabato aliambatana na diwani kata Bakoba Mhe. Shabani Rashidi pamoja na viongozi wa mtaa.
Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini akiambatana na Mhe diwani wa kata ya Bakoba na wananchi wa kata hiyo wakati wa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa
Social Plugin