Dar es Salaam 19 February 2024 – Katika jitihada za kuendeleza sekta ya habari nchini, Benki ya CRDB imeendesha semina maalum kwa wadau wa sekta ya habari nchini na uchumi “CRDB Bank Media Day” iliyofanyika katika Makao Makuu ya benki hiyo yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema “CRDB Bank Media Day” ya mwaka huu imejikita katika kuangazia ripoti ya Finscope 2023 na namna gani vyombo vya habari vinaweza kuchochea ujumuishi nchini.
“Ripoti ya Finscope ya 2023 inaonyesha ujumuishi wa kibenki upande wa huduma za benki ni 22% tu pamoja na jitihada na ubunifu mkubwa katika bidhaa. Hii inaonyesha kuna ombwe kubwa la elimu ya fedha, hivyo leo tumepata kujadili ninamna gani wenzetu wa sekta ya Habari wataweza kusaidia kutoa taarifa na huduma za fedha,” alisema Nsekela.
Katika semina hiyo waandishi wa habari walipata fursa ya kupata mafunzo ya namna ya bora ya kaandaa na kutoa mafunzo ya taarifa za biashara, fedha na uchumi. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kusaidia kujenga waandishi mahiri nchini.
Akizungumza katika semina hiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuandaa semina hiyo iliyowaleta wadau wa sekta ya habari kujadili namna ya kuongeza mchango wake katika maendeleo hususani katika kuongeza ujumuishi wa kifedha nchini. Matinyi amewahakikishia wadau wa sekta hiyo kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri yatakayosaidia kuboresha sekta ya habari.
Mada mbalimbali zimewasilishwa katika semina hiyo ikiwamo ‘Jukumu la Vyombo vya Habari katika kuchochea Ujumuishi wa Kifedha’ iliyowasilishwa na Mhariri Mstaafu wa Nationa Media Group Kenya, Charles Onyango Obbo, ‘Elimu ya Fedha kupitia Mitandao ya Jamii’ iliyowasilishwa na Fayness Sichwale amshauri wa masuala binafsi ya fedha na Mwanzilishi wa Personal Finance Hub, na Usomaji na Uwasilishaji wa Taarifa za Fedha’ iliyowasilishwa na Dkt. Ndalahwa Masanja, Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha ESAMI.
Katika Semina hiyo iliyohudhuriwa na waandishi na wahariri kutoka vyombo mbali nchini, Benki ya CRDB pia imezindua shindano maalum la kutafuta waandishi wahabari wachanga wa habari za biashara, fedha, na uchumi. Shindano hilo ambalo litaendeshwa kwa muda wa miezi miwili hadi Aprili 12 2024, litatoa washindi watatu ambao watajishindia zawadi ya Sh. Milioni 1 na nafasi ya kufanya kazi na Benki ya CRDB.
Aidha, katika hafla hiyo Benki ya CRDB imetoa tuzo za kutambua mchango wa waandishi wa habari wawili nguli katika sekta ya habari nchini. Waliokabidhiwa tuzo hizo ni Edda Sanga mwandishi mstaafu wa Shirika la Habari la Tanzania (TBC) na Mwenyekiti wa Umoja wa Waandishi wa Habri Wanawake (TAMWA), na Ndimara Tegambwage mwandishi wa zamani wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na moja ya waanzilishi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA).
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mobhare Matinyi, akimkaidhi Tuzo ya Heshima kutoka Benki ya CRDB kwa Mwanahabari wa Habari Mkongwe nchini, Mzee Ndimara Tegambwage , ikiwa sehemu ya kutambua mchango wake katika tasnia ya Habari hapa nchini, wakati wa semina maalum kwa wadau wa sekta ya Habari za uchumi nchini iliyoandaliwa na Benki va CRDB na kutamuliwa kama "CRDB Bank Media Day" ilivofanyika katika Makao Makuu ya benki hive yalivopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaii wa Benki va CRDB, Abdulmajid Nsekela, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki va CRDB Bruce Mwile pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki va CRDB, Tully Esther Mwambapa.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mobhare Matinyi, akimkaidhi Tuzo ya Heshima kutoka Benki ya CRDB kwa Mwanahabari wa Habari Mkongwe nchini Mama Eda Sanga, ikiwa sehemu ya kutambua mchango wake katika tasnia ya Habari hapa nchini, wakati wa semina maalum kwa wadau wa sekta ya Habari za uchumi nchini iliyoandaliwa na Benki va CRDB na kutamuliwa kama "CRDB Bank Media Day" ilivofanyika katika Makao Makuu ya benki hive yalivopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaii wa Benki va CRDB, Abdulmajid Nsekela, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Benki va CRDB Bruce Mwile pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki va CRDB, Tully Esther Mwambapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki va CRDB, Tully Esther Mwambapa akizunguma katika semina maalum kwa wadau wa sekta ya Habari za uchumi nchini iliyoandaliwa na Benki va CRDB na kutamuliwa kama "CRDB Bank Media Day" ilivofanyika katika Makao Makuu ya benki hive yalivopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam.
Social Plugin