Na Christina Cosmas, Morogoro
Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro limempa onyo diwani wa kata ya Kisaki Athuman Pande kutorudia kuzuia kamati ya fedha katika ukusanyaji wa mapato kwenye kata hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro Lucas Lemomo amesema hatua hiyo imekuja baada ya diwani huyo kukiri kufanya kitendo hicho baada ya kuitwa na kamati ya maadili.
Pia Lemomo amemsisitizia mkurugenzi wa halmashauri hiyo bi JoanFaith Kaleiya kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana na kamati ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Morogoro Rebecca Nsemwa amesisitizia wataalam wa afya kutoa elimu ya afya kwa wananchi ili kuchukua tahadhari ya kukabiliana na magonjwa ikiwemo kipindupindu na ugonjwa wa macho maarufu Red Eyes ambayo kwa sasa imekuwa ni tishio.
Social Plugin