Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA INA AKIBA YA KARATI MILIONI 37.46 ZA MADINI YA ALMASI

Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.

●Mgodi uligundulika mwaka 1940.

●Mpaka sasa mgodi una miaka 87 ya uchimbaji.

●Serikali inamiliki asilimia 25 ya hisa.

● Mgodi unaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 50 mbele.

Na.Samwel Mtuwa - Shinyanga

Tafiti zinaonesha kuwa kuna kiasi cha akiba ya karati milioni 37.46 za madini ya Almas katika mgodi wa almas wa Mwadui uliopo mkoani Shinyanga katika Wilaya ya Kishapu.

Hayo yamebainishwa leo Februari 18, 2024 na Kaimu Meneja wa Mgodi wa Almas Mhandisi Shaghembe Mipawa wakati akiwasilisha mada katika semina  kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini.

Mhandisi Mipawa ameongeza kuwa kisheria ukomo wa leseni  utakuwa mwaka 2033 ambapo   leseni itakuwa imemaliza muda wake lakini tafiti zinaonesha  rasilimali ya madini ya almas yaliyopo katika mgodi  yanaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 50 mbele hii ni kutokana makadirio ya rasilimali iliyopo.

Akielezea kuhusu umiliki wa mgodi Mhandisi Mipawa ameeleza kuwa kwasasa Serikali inaumiliki wa hisa kwa asilimia 25 na kampuni ya Petra Diamonds inaumiliki wa hisa kwa asilimia 75 ambapo mchango wa mgodi kwa jamii (CSR) ni asilimia 0.7 kwa mujibu wa sheria.

Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa ameeleza kuhusiana na mchakato wa kuongeza hisa za  umiliki kwa Serikali ambapo amesema kuwa Serikali  ipo katika majadiliano na baadhi ya taasisi za umma juu ya kuongeza hisa kufikia asilimia 37 kwa Serikali na asilimia  63 kwa kampuni ya Petra Diamond.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe.Kilumbe Ng'enda ameupongeza mgodi kwa kazi nzuri inayofanya ikiwa pamoja na kuitikia maelekezo yanayotolewa na Kamati katika kutekeleza majukumu yao.

Akitolea mfano juu ya Ujenzi wa Bwawa jipya  la maji taka (TSF) unaoendelea katika mgodi, hii ni ishara tosha kuwa mnasikiliza maelekezo kutoka kwa wajumbe wa kamati na kuyafanyia kazi ni imani yetu kuwa mtaendelea na utekelezaji wa maagizo mengine kama yatakavyotolewa kwenu.

Mgodi wa Almasi wa Mwadui uligundulika mwaka 1940 , una hekari za mraba 146 ukiwa ni moja ya mgodi mkubwa wa mwamba wa Kimberite duniani ambapo uchimbaji wake unafanyika kwa njia ya wazi yaani Open Pit.

#VISION2030:MadiniNiMaoshaNaUtajiri

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati kudumu ya Bunge Nishati na Madini Shabani Ngenda akizungumza wakati wa ziara hiyo- Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati kudumu ya Bunge Nishati na Madini Shabani Ngenda akizungumza wakati wa ziara hiyo
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa akizungumza wakati wa ziara hiyo
Kaimu Meneja wa Mgodi wa Almasi Mwadui Mhandisi Shaghembe Mipawa, ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Mgodi huo akiwaonesha wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini Shimo la kuchimba Madini ya Almasi.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini wakiwa kwenye Shimo la kuchimba Madini ya Almasi.
Muonekano wa sehemu ya Shimo la kuchimba Madini ya Almasi katika mgodi wa Mwadui
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Muonekano wa sehemu ya bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akielezea namna walivyojenga bwawa Jipya la kuhifadhia Majitope na kuanza uzalishaji wa Madini ya Almasi,mara baada ya bwawa la awali kupasuka.

Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kizalendo inayomilikiwa Watanzania ya City Engineering akielezea uimara wa bwawa jipya la tope laini katika Mgodi wa Williamson Diamond Limited.
Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kizalendo inayomilikiwa Watanzania ya City Engineering akielezea uimara wa bwawa jipya la tope laini katika Mgodi wa Williamson Diamond Limited.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Mhandisi Mkuu wa Mgodi wa Almasi Mwadui Shaghembe Mipawa akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.
Mwananchi akielezea namna walivyolipwa Fidia za Nyumba.

Afisa Mahusiano Mgodi wa Almasi Mwadui Benard Mihayo akitoa maelezo kwenye ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Nishati na Madini.

Muonekano wa sehemu nyumba zilizojengwa na Kampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kaya zilizoathirika na tukio la kupasuka kwa bwawa la Tope Laini

Picha na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com