BEI YA SUKARI, BARABARA , UCHAFU KWENYE MASOKO, VYOO, KIPINDUPINDU VYATAWALA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA

Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban Mwebea akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga ametoa onyo kwa Wafanyabiashara waliopandisha bei ya sukari kuacha mara moja ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria akisisitiza kuwa bei ya kilo moja ya sukari kwa bei ya reja reja ni shilingi 2800 hadi 3000 wakati bei ya jumla ni shilingi 2650 hadi 2800.

Kitinga ametoa onyo hilo leo Alhamisi Februari 15,2024 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichokuwa na ajenda ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa shughuli mbalimbali kutoka katika kata kwa robo ya pili ya mwaka 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

“Nitumie nafasi hii kuwaasa Wafanyabiashara tusijipangie bei za sukari zisizo na utaratibu, wasipange bei ambazo zipo nje ya utaratibu, tutapita kukagua nini kinaendelea kwenye maduka. Bei ya sukari bei elekezi iliyotolewa ni 2650 hadi 2800 bei ya rejareja na bei ya jumla shilingi 2800 hadi 3000”, amesema Kitinga.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga.

“Kipindupindu bado kipo tuendelee kuhimiza masuala ya usafi, tufuate taratibu za afya bora na tuhakikishe wananchi wawe na vyoo vitumike vizuri na tuendelee kugawa dawa za kutibu maji ili kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu”,ameongeza Kitinga.

Wakiwasilisha taarifa za kata, Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wamezitaja baadhi ya changamoto kubwa zilizopo kwenye kata zao kuwa ni uharibifu wa miundombinu ya barabara uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha, ukosefu wa vivuko na mitaro kwenye baadhi ya maeneo ,upungufu wa maabara, matundu ya vyoo, walimu kwa baadhi ya shule pamoja na kukosekana kwa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo , upungufu wa watendaji katika baadhi ya kata pamoja.

Pia Madiwani wamewataka wafanyabiashara wa chakula kuacha tabia ya kumwaga maji machafu 'ukoko' barabarani pamoja watendaji wa Halmashauri kuhakikisha hakuna uchafu kwenye masoko pamoja na uchafu kuzolewa kwa wakati ili kuepuka ugonjwa wa Kipindupindu.
Diwani wa kata ya Mwamalili Mhe. James Matinde Furushi akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Zamda Shaban Mwebea amewataka madiwani kuhakikisha wanafuatilia zoezi la wanafunzi kuripoti katika shule zilizopo katika kata zao pamoja na mkurugenzi kuhakikisha wanaharakaisha kuanza kwa matumizi ya kituo cha magari cha Kambarage hatua itakayorahisisha huduma kwa wananchi.

“Suala la usafi hasa kwenye masoko yetu bado ni tatizo, ni kweli masoko yetu yamekuwa siyo masafi kwa sasa, hivi sasa hali siyo nzuri ukilinganisha na zamani. Hali ya masoko siyo nzuri, hawa akina mama wanaopika chakula wanamwaga maji hovyo mfano pale Nguzo Nane na Kambarage. Tukazie usafi kwenye maeneo ya usafi na maeneo mengine, taka zizolewe kwa wakati ili kuepuka magonjwa kama Kipindupindu”,amesema Mwebea.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban Mwebea.

Katika hatua nyingine Mwebea amewataka madiwani kupendana, kushirikiana, kuheshimiana na wadumishe upendo kila mmoja kwa nafasi yake ili kutimiza adhma ya serikali yetu ya kuwaletea maendeleo wananchi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze amesema wanaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kutatua changamoto ambazo zimeelezwa na madiwani huku akibainisha kuwa licha ya uwepo wa changamoto hizo kuna baadhi ya maeneo ambayo yameelezwa kuimarika ikiwa ni pamoja na eneo la ulinzi na usalama,upimaji wa ardhi na ufikishwaji wa nishati ya umeme kwa baadhi ya maeneo na ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo, shule mpya na Stendi ya Mabasi ya Kambarage.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord Makombe amesema changamoto nyingi zimepungua hivyo kuwataka Madiwani na watendaji kuendelea kushughulikia changamoto za wananchi.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban Mwebea akizungumza wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Februari 15,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Februari 15,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Februari 15,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwalimu Alexius Kagunze akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Alhamisi Februari 15,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Anord. Makombe akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Msimamizi wa Idara ya Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga na Ezra Manjerenga akitoa ufafanuzi kuhusu ndege wanaoharibu mazingira eneo la Nguzo Nane  kwenye kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Kata ya Kambarage Mhe. Hassan Mwendapole akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Kata ya Old Shinyanga Mhe. John Lyeta akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Kata ya Kolandoto Mhe. Mussa Elias akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Viti Maalumu , Mhe. Shela Mshandete akiwasilisha taarifa ya kata ya Mjini kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani viti maalumu manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri akiwasilisha taarifa ya kata ya Ibadakuli kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga

Diwani wa Kata ya Kitangili Mhe. Mariam Nyangaka akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Kata ya Ngokolo Mhe. Victor Mkwizu akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Kata ya Masekelo Mhe. Peter Koliba akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Viti Maalumu Mhe. Pika Chogello akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Kata ya Chibe Mhe. John Kisandu akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Diwani wa Kata ya Lubaga Mhe. Reuben Doto akiwasilisha taarifa ya kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Watendaji wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post