RC MNDEME AWASIMAMISHA KAZI VIGOGO WANNE IDARA YA ARDHI KAHAMA....AAGIZA POLISI KUKAMATA WAUZAJI NA WATEJA BIASHARA YA NGONO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi kutoka mmoja wa wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Kahama

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameendelea na ziara ya kupokea, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambapo leo amekutana na wananchi wa Manispaa ya Kahama ambapo kero zilizotawala ni kuhusu migogoro ya ardhi lawama nyingi zikitolewa Ofisi ya ardhi Manispaa ya Kahama hali iliyomlazimu kuchukua hatua ya kuwasimamisha kazi viongozi wanne wa Idara ya Ardhi wapishe kwa ajili ya uchunguzi kwanini kuna migogoro mingi ya ardhi.

Akizungumza katika mkutano wake na wananchi uliofanyika katika viwanja vya Parking ya Malori katika kata ya Majengo Manispaa ya Kahama, Mhe. Mndeme amewasimamisha kazi viongozi wanne wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kutokana na tuhuma mbalimbali za migogoro ya ardhi wanazohusishwa nazo kinyume cha maadili ya kazi.

"Malalamiko mengi Kahama ni ardhi, ardhi, ardhi, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  anataka wananchi waishi bila migogoro, waishi kwa amani na usalama, hakuna aliye juu ya sheria. Viongozi wengi wamekuja hapa kero kubwa ni ardhi, huko ardhi kuna nini?, baada ya kuona ardhi ni changamoto kubwa hapa Kahama.,Nimeamua kuwasimamisha kazi viongozi wanne Idara ya ardhi Manispaa ya Kahama ambao ni Clemence Mkusa (Mkuu wa Idara ya Ardhi), Yusuph Shaban Luhumba (Afisa ardhi mteule), Yahaya Msangi (Mpima ardhi) na Crispine Kisengo (Afisa Mipango Miji).

"Naagiza wasimame kazi ,watupishe kwanza tufanye uchunguzi kwanini migogoro ya ardhi Kahama haiishi. Tutaleta tume hapa, itafanya kazi, itachunguza, ikiwakuta wana hatia basi taratibu zingine za kinidhamu na kisheria zitafuata, ikiwakuta wako vizuri wataendelea na majukumu yao. Kwa hiyo naomba hawa watumishi wanne wa Idara ya Ardhi watupishe kwanza tuwafanyie uchunguzi. 

Na wanasimama kazi kuanzia leo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo simamia hili, unda tume ije ichunguze tuone tatizo ni nini. Haiwezekani kila siku, ardhi, ardhi, ardhi na tumeona mengine sehemu zingine hati zinatolewa mara mbili mbili, sehemu zingine mtu anaruhusiwa kulipa lakini hapewi hati, sehemu zingine analipa lakini lile eneo lina mtu mwingine, mambo yamechanganyika changanyika", amesema Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mhe. Mndeme pia ametatua mgogoro wa ardhi wa Bi. Caroline Magege uliodumu kwa muda wa miaka sita na kuupatia ufumbuzi mgogoro wa ardhi wa bi. Maimuna Misana huku akiwataka watumishi wa Idara ya Ardhi kuzingatia maadili ya utumishi na kuacha dhuluma dhidi ya wananchi.

Mbali na migogoro ya ardhi ikiwemo ya Maimuna Misana na  Caroline Dotto Magege iliyochukua muda mrefu kupatiwa ufumbuzi, kero zingine ni ubovu wa barabara na mitaro kata ya Majengo hali inayosababisha maji kuingia kwenye nyumba za watu pindi mvua inaponyesha, ukosefu wa huduma ya maji kwenye baadhi ya maeneo pamoja na uhalifu kwenye baadhi ya maeneo likiwemo eneo la Majengo linalodaiwa kuwa na vibaka huku wanawake wanaofanya biashara ya ngono wakihusishwa na vitendo vya wizi.

Mhe. Mndeme ameliagiza jeshi la polisi kufanya doria za mara kwa mara ili kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ngono pamoja na wateja wao kwani serikali hairuhusu biashara hiyo haramu.

“Naliekeza Jeshi la Polisi kufanya doria za mara kwa mara kwenye maeneo yote ambako panafanyika biashara ya ngono, kamateni anayefanya biashara ya ngono, mteja wake, mlinzi wake pamoja mmiliki wa nyumba inayohifadhi wanafanyabiashara ya ngono. Tunataka kila mmoja afanye kazi halali,wengine wanajificha kwenye biashara hii na kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi. Bidhaa na mnunuzi wa biashara ya ngono wote kamata, wanaowahifadhi nao kamateni”,amesema Mhe. Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi kutoka mmoja wa wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi kutoka mmoja wa wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi ya Maimuna Misana (aliyesimama)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi ya Maimuna Misana (aliyesimama)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameshikilia hati wakati akisikiliza kero ya ardhi ya Maimuna Misana (aliyesimama kushoto)
Caroline Dotto Magege akielezea kero ya mgogoro wa ardhi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero ya ardhi ya Caroline Dotto Magege (aliyesimama kushoto)

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza kero za wananchi katika Manispaa ya Kahama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post