Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifurahia jambo wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amefanya mkutano wa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga ambapo miongoni mwa malalamiko mengi ya wananchi ni kuhusu migogoro ya ardhi, mirathi, kazi, mafao, kupanda kwa bei ya sukari, mikopo umiza, ujenzi wa masoko kutokamilika, biashara, elimu, umeme, kutelekeza familia na watoto,miundombinu ya barabara ubovu wa miundombinu ya barabara hasa ya kutoka Ndala kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Mwawaza.
Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Februari 28,2024 katika Stendi ya Magari madogo iliyopo Soko Kuu kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka Watumishi wa Serikali wafanye kazi kwa weledi katika kuwahudumia wananchi huku akiwasisitiza Watumishi wa Idara ya Ardhi kufanya kazi zao kwa weledi na umakini ili kuepusha migogoro ya ardhi, ikiwamo kutogeuza matumizi ya ardhi kinyume na utaratibu.
Amesema suala la Umeme siyo anasa hivyo ameiagiza TANESCO kuhakikisha inapeleka umeme katika eneo la Nyanhende kabla ya Mwezi Aprili mwaka huu ambapo kuna malalamiko ya wananchi kutopatiwa huduma hiyo licha ya nguzo za umeme kupelekwa.
Mhe. Mndeme pia ,ameitaka TARURA kuhakikisha inatengeneza mitaro na kutengeneza barabara zilizoharibiwa na mvua huku akihimiza wananchi kutunza na kulinda miundombinu ya maji na umeme.
Kuhusu kupanda kwa bei ya sukari, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amesema bei elekezi iliyotolewa na serikali ni kuanzia shilingi 2,800/= hadi 3,000/= kwa kilo moja na si vinginevyo na kwamba serikali inaendelea kuchukua hatua kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari na kupandisha bei ya sukari.
Kwa upande mwingine Mhe. Mndeme amewataka wanaume kuacha kutelekeza watoto badala yake pindi wanapowapa mimba wanawake wawatunze na kulea watoto pamoja.
Akijibu kero ya kutokamilika kwa ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga, ametoa maelekezo kwamba hadi kufikia Mei 30 mwaka huu Soko hilo liwe limeshakamilika kujengwa lote na kuanza kutumika, na siyo Mwezi Julai kama alivyosema Mkurugenzi.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya sekta ya elimu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu na vyoo, hivyo kuwataka wazazi kupeleka watoto shule.
“Pochi ya mama imefunguka, katuletea shilingi Bilioni 56 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu. Wazazi pelekeni watoto shule badala ya kuwaacha wanazurura mtaani na wengine kufanya biashara ya kuuza chai na vitumbua”,amesema.
Akijibu swali la mwananchi kuhusu maendeleo ya Timu ya Stand United, Mhe. Mndeme amesema, Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imejipanga vizuri kuhakikisha timu hiyo inapanda daraja.
“Tutahakikisha Stand United inaingia Ligi Kuu, kwa pamoja tuimarishe nguvu ili Timu hii irudi. Tunataka Ligi kuu ichezwe Shinyanga, nah ii inawezekana kwa sababu nia tunayo, nguvu tunayo, sababu tunayo na uwezo tunao”,ameongeza Mhe. Mndeme.
“Kero zote ambazo mmeziwasilisha hapa zitashughulikiwa kwa utaratibu na kila mtu atapata haki yake,”amesema Mndeme akifunga mkutano huo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema jeshi hilo la polisi linaendelea kuchukua hatua kwa madereva wa mabasi wanaokiuka sheria za usalama barabarani ikiwemo kuendesha kwa kasi kubwa wanapoingia Mjini Shinyanga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, akijibu kero ya Mikopo umiza, amewatahadharisha wananchi kuhusu mikopo umiza inayofanywa mtaani na kuwataka kutafuta mikopo kwenye taasisi za Kibenki na pindi dirisha la mikopo ya halmashauri itakapofunguliwa wajitokeze kupata mikopo isiyo na riba kwani lengo la serikali ni kuhakikisha inamkomboa mwananchi kiuchumi.
Amewataka wananchi wajiepushe na Taasisi ambazo zinakopesha fedha zisizo na vibali wala kutambulika na BOT, na kwamba watakapopata taarifa za Taasisi isiyosajiliwa wampatie taarifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumatano Februari 28,2024 katika Stendi ya Magari madogo Soko Kuu - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifurahia jambo wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiandika dondoo muhimu wakati akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akisikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi katika Manispaa ya Shinyanga