Na Christina Cosmas _ Morogoro
Juhudi za kumwezesha mtoto wa kike zinapaswa kuenda sambamba na kumwendeleza mtoto wa kiume ili kuwapa umoja utakaowainua katika mambo mbalimbali kijamii, kisiasa na hata kiuchumi na kukamilisha dhana ya hamsini kwa hamsini.
Meneja wa Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Morogoro Joan Nangawe amesema hayo jijini Dar es salaam wakati wa kuanzishwa kwa tawi la vijana katika chemba ya biashara ya wanawake(TWCC) mjini hapa.
Anasema tawi hilo ni njia nzuri ya kuwezesha vijana wa kike na wa kiume kupata fursa mbalimbali za kibiashara.
Hivyo Nangawe amepongeza Uongozi wa Chemba ya Biashara ya wanawake kwa kuliona suala la vijana kwa pande zote na kutambua kuwa maendeleo ya mwanamke na ujenzi wa familia bora unakuwa mzuri pale ambapo kijana wa kiume atashirikishwa na kushirikiana na kijana wa kike.
Hivyo anasema wao kama wadau muhimu wanaendelea kuwatia moyo vijana kushirikiana kwa maendeleo endelevu ya kizazi kijacho.
Social Plugin