RUWASA YASAINI MIKATABA 7 YA UJENZI WA MIRADI YA MAJI VIJIJI 17 SHINYANGA... RC MNDEME ATAKA UBORA KWA WAKATI MABOMBA YASIPASUKE

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Na Kadama Malunde _ Malunde 1 blog

Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga imetia saini Mikataba 7 na Wakandarasi yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.443 Tsh (6,443,108,866.76/=) kwa ajili ya kutekeleza miradi sita ya maji na mmoja kwa ajili ununuzi wa bomba na vifaa vya ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji 17 mkoani Shinyanga.

Hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imefanyika leo Jumatatu Februari 5,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ikishuhudiwa na wadau mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Akitoa taarifa, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela amesema kipindi cha Julai – Desemba 2023 RUWASA imeshatangaza jumla ya Zabuni 9 ikihusisha ujenzi wa miradi nane na zabuni moja kwa ajili ya bomba na vifaa mbalimbali vya ujenzi wa miradi minne itakayotekelezwa mfumo wa Force Account ambapo hadi sasa zabuni 7 tayari mchakato wake umekamilika na ndiyo utiaji saini wa mikataba hiyo umefanyika na miradi miwili ipo katika hatua za manunuzi.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.
 
"Katika zabuni saba zilizotangazwa ngazi ya mkoa na mchakato wake umekamilika zina thamani ya shilingi 6,443,108,866.76/= pamoja na Kodi ya ongezeko la thamani (VAT). Mikataba hii ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika vijiji 17 ikitekelezwa na Wakandarasi Jonta Investment Ltd katika wilaya ya Kahama, Otonde Construction & General Supplies Ltd katika wilaya ya Shinyanga pamoja na Corsyne Consult Ltd na Geospatial Classic Works Ltd katika wilaya ya Kishapu na kwa upande wa ununuzi wa bomba na viungio katika wilaya za Kahama, Shinyanga na Kishapu Mzabuni ni Hazglobal Logistics Co. Ltd", ameeleza Mhandisi Payovela.

Ameitaja miradi itakayotekelezwa kuwa ni Ujenzi wa Mradi wa maji katika vijiji vya Chona, Ubagwe na Bukomela katika Halmashauri ya Ushetu, ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji vya Ng'wampangabule, Zumve, Jimondoli na Sumbigu katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na ujenzi wa mradi wa maji katika vijiji vya Ipeja, Itilima, Ikonokelo na Ikoma halmashauri ya Kishapu.

"Pia kuna ujenzi na upanuzi wa mradi wa maji Nhobola, ujenzi wa mradi wa maji Nyenze - Ng'wang'holo kwenda Kabila na ujenzi na upanuzi wa mradi wa Maji kwenda vijiji vya Wela, Wila, Mwataga na Mwanhulu",amesema Mhandisi Payovela.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela (kushoto) na  Wakandarasi/Wazabuni baada ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024 

Katika hatua nyingine, amesema RUWASA Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imepanga kutumia shilingi 28,990,202,843.41/= kwa ajili ya shughuli mbalimbali za utekelezaji wa miradi ikiwemo 33 ambapo kati ya miradi 14 ni ya ukamilishaji, miradi mipya 15 itajengwa na miradi 4 ya kutafuta vyanzo vya maji na usanifu.

"Kipindi cha Julai-Desemba 2023 miradi minne ilikamilika, miradi inayoendelea kwa sasa ni 10 yenye thamani ya shilingi 29,534,486,729.85/= katika vijiji 36. Hadi kufikia Januari 31,2024 mkoa wa Shinyanga umepokea shilingi 13,794,821,497.54/= sawa na asilimia 48 ya bajeti. Fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya madai ya Wakandarasi, usimamizi wa miradi, uendelevu wa miradi na matumizi mengineyo",amefafanua Mhandisi Payovela.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme watumishi, watalaamu na wazabuni kuhakikisha miradi ya maji inatekelezwa kwa viwango na ubora unaotakiwa kwani matarajio ni kuona miradi hiyo inachochea maendeleo ya mkoa wa Shinyanga.

“Ubora wa kazi ya Wakandarasi ikaonekane, wakandarasi vaeni uzalendo, tunataka miradi ikamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa, tupate mabomba bora yasiyopasuka, kusiwe na upotevu wa maji kwani mabomba yanapopasuka wakati mwingine inasababisha maji yasiwe salama”,amesema Mhe. Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya miradi ya maji

“Lengo la serikali ni kuona wananchi wapatiwa maji safi na salama, tunataka kumtua mwanamke ndoo kichwani, tunataka mwanamke atumie muda mfupi kupata huduma ya maji. Hivyo hakikisheni miradi hii pia inakuwa endelevu kwa ajili ya vizazi vijavyo”,ameongeza Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika hatua nyingine amempongeza Meneja RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela pamoja na watendaji wa RUWASA kwa kazi nzuri wanayoifanya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo mkoani Shinyanga huku akiongeza kuwa utekelekezaji wa miradi hiyo ikiwemo ya maji ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Naye Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani amesema miradi hiyo ya maji inaenda kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Halmashauri ya Ushetu.

“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea fedha kwa ajili ya miradi ya maji. Rais Samia ni Mama wa fedha. Ushetu tupo vizuri, tumesimama na mama na tutakufa na mama. Wakandarasi nendeni mkafanye kazi kwa ufanisi sisi tunataka maji”,ameeleza Mbunge Cherehani.

Akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi waliosaini mkataba, Stephen Owawa kutoka Kampuni ya Geospatia Classic Works Ltd ameahidi kuwa wataenda kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa na kwa wakati.

“Tunashukuru sana Wakandarasi Wazawa kupewa kazi ya kutekeleza miradi hii, hatutawaangusha, mabomba hatayapasuka, maji hayatapotea. Tunaomba ushirikiano kwa viongozi na wananchi ili kuhakikisha miradi inatekelezwa ndani ya muda uliopangwa ikiwezekana mingine chini ya muda uliopangwa”,amesema Owawa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024 iliyofanyika leo Jumatatu Februari 5,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024 iliyofanyika leo Jumatatu Februari 5,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga

Zoezi kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024  kati ya RUWASA na Wakandarasi/Wazabuni likiendelea 

Picha ya kumbukumbu Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela (kushoto) na Wakandarasi/Wazabuni baada ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024 

 Mkandarasi Stephen Owawa kutoka Kampuni ya Geospatia Classic Works Ltd akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi waliosaini mikataba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akizungumza wakati wa hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Wadau wa maji wakiwa katika hafla ya kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji mkoani Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post