Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Februari 7,2024
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Februari 7,2024
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imejipanga kufuatilia fedha za miradi ya maendeleo ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa thamani halisi ya fedha kama serikali ilivyokusudia.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatano, Februari 7,2024 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga, Donasian Kessy amesema miongoni mwa mikatati yao ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024 ni kufuatilia fedha za miradi pamoja na kufanya warsha na kusimamia utekelezaji wa maazimio yote ya changamoto mbalimbali zilizobainika kwenye chambuzi za mifumo na miradi ya maendeleo.
Katika hatua nyingine amesema katika kipindi cha robo ya pili yam waka wa fedha 2023/2024 TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga ilifanya ufuatiliaji wa miradi ya SEQUIP (Mpango wa Uboreshaji wa elimu ya Sekondari) ili kuona kama miradi inatekelezwa kwa wakati na katika ubora na viwango vinavyotakiwa.
“Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkoa wa Shinyanga ulipokea shingi Bilioni 5.2 (5,283,343,372/=), fedha hizi zilikuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa miradi 13 ambayo ni shule mpya sita za sekondari, ujenzi wa nyumba sita 2 in 1 za walimu na ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa”,amesema Kessy.
“TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga iliweza kufanya ufuatiliaji wa miradi 10 ya SEQUIP yenye thamani ya Shilingi 4,063,343,372/= na kujiridisha kuwa mbali na uwepo wa changamoto zinazorekebishika, miradi hiyo imetekelezwa kwa ufanisi na ubora unaotakiwa na miradi hiyo kama shule na nyumba za walimu imeshaanza kutumika”,ameongeza Kessy.
Ametoa wito kwa wananchi kushiriki zaidi katika usimamizi wa miradi ya maendeleo kwani baadhi ya utekelezaji wa miradi ya SEQUIP imeshirikisha jamii hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi.
Aidha amesema pia walifuatilia miradi miwili ya sekta afya inayotekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Msalala yenye thamani ya shilingi Milioni 700 ambapo dosari ndogo ndogo zilibainika kwenye miradi na ushauri ulitolewa wa kutatua dosari hizo.
Social Plugin