Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TGNP NA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA WAENDESHA MAFUNZO YA JINSIA


Na Deogratius Temba

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) wameendesha mafunzo ya urasimishaji wa masuala ya Kijinsia kwa watumishi wa Halmashauri 10 katika ngazi ya Kata.

Mafunzo hayo ni sehemu a mradi unaofadhiwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake (UNwomen) unaojulikana kama Sauti ya Wanawake, Uongozi na Haki za kiuchumi unaotekelezwa katika mikoa na Halmashauri mbalimbali kwa lengo la kuwapa wanawake nafasi ya kupaaza sauti zao, ushiriki kwenye uongozi na haki ya kunufaika na fursa za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi, amesema kwamba mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo maafisa wa Halmahauri wanaofanya kazi katika ngazi ya Kata ambako kuna wajamii ili waweze kushirikisha jamii kikamilifu katika mchakato wa kuandaa mipango ya serikali ngazi ya Kata na vijiji

“Tumeandaa mafunzo haya baada ya kutambua kwamba, wapo maafisa katika ngazi ya chini ya mamkala za serikali za Mitaa, ambao wakielewa masuala ya Kijinsia wataweza kuvipa nafasi vipaumbele vya Kijinsia katika ngazi ya Jamii, wakati wa kuibua, pia wana nafasi kubwa ya kusimamia mchakato wa O&OD ukawa shirikishi Zaidi na wenye manufaa kwa jamii” alisema Lilian

Aidha ameongeza kwamba, washiriki wa mafunzo hayo kutokana na umuhimu wao na nafasi walizo nazo katika ngazi ya jamii, wanauwezo wa kutoa elimu katika jamii kupitia mikutano ya vitongoji na vijiji ili kuwafanya wanawake washiriki lakini pia kujitokeza kugombea uongozi ili kuongeza idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi ngazi ya Kijij na mtaa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Naibu Mkuu wa Chuo, Utawala na Fedha, Dkt Lazaro Kisumbe, Alisema kwamba, Chuo hicho kilifanya utafiti na kubaini kwamba kuna mapungufu ya Kijinsia katika mamlaka za serikaali za Mitaa, ambayo yanakwamisha jitihada za serikali katika kupanga mipango na bajeti yenye mtazamo wa Jinsia.

“ Mradi huu, unalenga kuondoa hili pengo la Kijinsia katika jamii, ndio maaana kwa kushirikiana na Shirika la UNWomen na TGNP tunalenga kujenga uwezo kwa wataalamu hawa ngazi ya kata, ili wanaaporudi wakatoe elimu hiyo kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) namna ya kuzungatia usawa wa Kijinsia wakati wa kuandaa mipango lakini pia kuweka nguvu kwenye vipaumbele vya Jamii” alisema.

Alisema kwamba, kupitia mafunzo hayo, wataalamu hao ngazi ya Kata, watawezesha kutambua mbinu za kwenda kukondoisha masuala ya Kijinsia katika ngazi ya Kata, na kuhaikisha wanawezesha masuala ya Kijinsia kueleweka katika ngazo zote.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com