NA ELISANTE KINDULU, CHALINZE.
SHULE ya sekondari ya Kimataifa ya Imperial imeitembelea shule ya msingi ya Ridhiwani Kikwete kwa lengo la kufanya hisani katika siku ya wapendanao leo tarehe 14 mjini Chalinze.
Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ridhiwani Kikwete kwa shule hiyo ya Imperial kuwapatia wanafunzi wa Ridhiwani Kikwete zawadi mbalimbali zikiwemo sabuni, nguo, soksi, sweta, viatu na madaftari.
Aidha Shule ya Sekondari Imperial na Shule ya Awali na Msingi ya Ridhiwani Kikwete wamekubaliana kufungua mahusiano ya kitaasisi katika nyanja ya Sanaa na michezo ambapo kutakuwa na mpango wa kujengeana uzoefu katika masuala mbalimbali ya Sanaa na michezo kwa siku zijazo.
Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na walimu na wanafunzi wa shule zote mbili zilizopo katika halmashauri hiyo ya Chalinze katika mkoa wa Pwani.
Social Plugin