Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MALALAMIKO YA WANANCHI YANATOKANA NA WATUMISHI KUKOSA UADILIFU KWENYE KUTOA HAKI - DC MKUDE




Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Modest Mkude amezishauri taasisi zote wilayani humo kufanya kazi kwa uwajibikaji,weledi na uadilifu.

Mkude ameyasema hayo leo Februari 1,2024 alipokuwa mgeni wa heshima kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo yenye kauli mbiu "Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa taifa nafasi ya nahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai".

Aidha amesema malalamiko mengi kwa wananchi ni kutokana baadhi ya watumishi kutotimiza wajibu wa utoaji haki kwa wakati na    wanatakiwa kuwapenda,kuwasikiliza maoni yao na kuwatumikia watu wote bila kujari itikadi na mitazamo yao.

"Ndugu zangu natoa wito huu si tu kwa watumishi wa mahakama kwa kuwa tuko kweye viwanja hivi kusherehekea wiki yao ya sheria tukumbuke utumishi ni wito na wakati mwingine unawezalaumiwa hata hujakosea ila wajibu mkubwa tulionao ni kuwatumikia wananchi na kuwapa haki yao kwa hiyo uhimilivu na usitahimilivu ni muhimu sana kwetu kauli mbiu hizi tusiziimbe tu bali tuzitendee kazi" amesema Mkude.

Sambamba na hayo ameongeza kwa kutoa wito kwa wananchi na wadau wengine kuwa mahakama ni chombo muhimu kwa sababu ya uwepo wa utawala bora na chombo hicho hakiwezi kufanya kazi peke yake bila ushirikiano wa wadau mbalimbali.

Hata hivyo akisoma hotuba mbele ya mgeni wa heshima na wageni waalikwa, mgeni rasmi wa sherehe hizo ambae pia ni hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Kishapu bi.Johanitha Projest Rwehabula  amesema mahakama ni muhimili wenye mamlaka ya mwisho ya utoaji haki kwa mjibu wa ibara ya 107 a(1) (d) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Pia amesema mfumo wa kielektroniki umeanzishwa ambao unatoa huduka za usajili wa mashauri kwa njia ya mtandao,upangaji wa mashauri kwa majaji na mahakimu,uandishi wa mienendo na hukumu kwenyw mfumo nakuwezesha mifumo ya wadau ikiwemo NIDA,NPS na RITA kusomana.

"Kutokana na mahakama kupiga hatua katika kipengele cha TEHAMA wadau wanao wajibu kutekeleza wajibu wao ili uwekezaji uliofanywa uwe na maana hiyo itasaidia kupata haki kwa wakati kama ambavyo mahakama imedhamiria" ,amesema hakimu Rwehabula
Mgeni rasmi wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria ambaye ni hakimu mkazi mfawidhi  wilaya ya Kishapu bi. Johanitha Projest Rwehambula akisoma hotuba mbele ya mgeni wa heshima na wageni waalikwa leo Februali 1,2024 sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Modest Mkude Mgeni wa heshima akitoa hotuba fupi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama ya wilaya Kishapu leo Februari 1,2024
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Modest Mkude Mgeni wa heshima akitoa hotuba fupi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama ya wilaya Kishapu leo Februari 1,2024
Mwakilishi wa ofisi ya taifa ya Mashtaka wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Wakili Groria Ndondi  akisoma hotuba fupi siku ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama Kishapu.
Mgeni wa heshima Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akiteta jambo na mgeni rasmi ambaye ni hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Bi. Johanitha Projest Rwehabula wakiwa kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama  ya wilaya Kishapu 
Baadhi ya wadau wa mahakama wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi bi. Johanitha Projest kweye sherehe ya kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika leo katika viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya msingi Buduhe na Kishapu sekondari wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika leo kwenye viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo.

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambao pia ni wadau wa hakijinai wakiwa kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika leo katika viwanja vya mahakama ya wilaya Kishapu.
Watumishi wa mahakama wilayani Kishapu mkoani shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika leo katika viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo.
Watumishi wa mahakama wilayani Kishapu mkoani shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria yaliyofanyika leo katika viwanja vya mahakama ya wilaya hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com