Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA TAIFA YA USHIRIKA KUZINDULIWA MEI MWAKA HUU

 

MRAJIS na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati akifungua kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

MRAJIS na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege,akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

BAADHI ya Washiriki wakimsikiliza Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, wakati akifungua kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

KAIMU Naibu Mrajis -Uhamasishaji Bi.Consolata Kiluma,akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

NAIBU Mrajis wa Vyama vya Ushirika – Udhibiti Bw. Collins Nyakunga,akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Shirikisho wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Charles Jishuli,akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Bodi Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Bw.Cuthbert Msuya,akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

MRAJIS Msaidizi wa Vyama vya kifedha kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Josephat Kisamalala,akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kilichofanyika leo Februari 27,2024 jijini Dodoma.

Na Alex Sonna-DODOMA

MRAJIS na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amesema Benki ya Taifa ya Ushirika inatarajiwa kuanza kazi Mei mwaka huu ambapo kwa sasa wapo katika mchakato wa upatikanaji wa leseni.
Dkt.Ndiege ameyasema hayo leo Februari 27, 2024 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi kati ya TCDC,Vyama vya Ushirika na Benki ya KCBL kwa lengo la kuongeza uwekezaji kwa Wanaushirika Wanahisa kufikia asilimia 51.
Amesema wamekubaliana Benki ya Taifa ya Ushirika itamilikiwa na wanaushirika kwa kumiliki asilimia 51 ya Hisa zote.
Hisa asilimia 49 itamilikiwa na watu wengine ambao sio wanaushirika na ndio wanaona umuhimu kwa kununua Hisa kwa wingi ukilinganisha na Wanaushirika.
"Mpaka Sasa wanaushirika wamenunua Hisa asilimia 48 ili kufikia kwenye asilimia 51 ili benki hii izinduliwe mwezi wa tano mwaka huu.
Amesema kwa sasa zinahitajika Bilioni 2.8 kutoka kwa Wanaushirika ili kuweza kufikia asilimia 51 ambayo itawapa umiliki wa benki hiyo.
Dkkt. Ndiege amesema Wanaushirika wanamshukuru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hayati Anne Mgwira, kwa kupambana kuhakikisha benki ya KCBL inaendelea kuwepo.
"Kuna mambo mengi yamefanyika tumekutana mara nyingi kuhakikisha hili zoezi tunalikamilisha. Nichukue nafasi hii kuwapongeza hatua tuliyofukia kila mtu anatutamani leo hii tukisema BoT tupeni leseni wanatupa na tunaanza," amesema Mrajis.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Charles Jishuli, amesema benki hiyo mchakato umeanza muda mrefu na bahati nzuri Mrajis aliyekuja anaufahamu.
"Mrajis umefanya msukumo mkubwa na hatuna budi kukupongeza," amesema Jishuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com