Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA NBC YATOA MAFUNZO YA FEDHA KWA WACHEZAJI WA STAND UNITED

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Benki ya Taifa ya Biashara ya NBC tawi la Shinyanga imetoa Elimu ya Fedha kwa Wachezaji wa Timu ya Stand United ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya fedha.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Alhamisi Februari 1,2024 katika Benki ya NBC tawi la Shinyanga yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya fedha, kuimarisha ushirikiano na kufahamiana.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja amesema Benki ya NBC ambayo ni Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) na NBC Championship imewashauri wachezaji wa Stand United kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Benki hiyo ikiwemo Bima za afya na vyombo vya moto, mikopo pamoja na akaunti mbalimbali ikiwemo Akaunti ya Mshahara, Akaunti ya Kua Nasi, Akaunti ya Malengo, Akaunti ya NBC Direct na huduma za NBC Wakala.

Amewashauri wachezaji hao kujiwekea utamaduni kwa kujiwekea akiba na uwekezaji pamoja na kuwa na bima katika Benki ya NBC wanaposajiliwa na timu mbalimbali.

“Tumekutana hapa leo ili kutoa mafunzo ya huduma za kifedha kwa wachezaji wa Stand United ili kuimarisha mahusiano na timu hii, tutaendelea kushirikiana ili kuhakikisha tunatatua changamoto zinazoikabili timu hii.

Tunazo huduma nyingi za kifedha. Karibuni Benki ya NBC pia mfurahie njia mbadala za kupata huduma za kibenki ‘Benki Kidijitali na NBC’ bila ulazima wa kufika kwenye tawi kwa kupiga *150*55# au kupitia App ya NBC Kiganjani”,amesema Chagonja.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja.

Katika hatua nyingine amesema Benki ya NBC ina jumla ya matawi 57 nchi nzima, ATM 197 na zaidi ya mawakala 11,000 ikihudumia makundi matatu ya wateja wakiwemo watu binafsi, wateja wa kati na wateja wakubwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Stand United ya Mkoa wa Shinyanga inayoshiriki Ligi ya Championship, Stivian Antidius (Wenger) ameishukuru Benki ya NBC kwa kuwapatia elimu ya fedha wachezaji na viongozi wa timu hiyo huku akiiomba Benki hiyo kuisaidia kwa chochote timu hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali hasa katika kipindi hiki ambacho wana mechi 13 mbele yao.

“Tunawashukuru sana NBC na wadhamini wetu Jambo kwa ushirikiano wanaotupatia, tunaomba wadau wengine katika mkoa wa Shinyanga na nje ya Shinyanga mjitokeze kutusaidia kwani tunakabiliwa na changamoto mbalimbali”,amesema Antidius

Nao washiriki wa mafunzo hayo, wameishukuru Benki ya NBC kwa kuwajali na kuwapata mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kuwa na nidhamu ya fedha lakini pia kuweka akiba na kuwekeza kupitia benki hiyo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja akizungumza wakati wa mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na Viongozi wa Stand United leo Alhamisi Februari 1,2024 katika Benki ya NBC Tawi la Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Bi. Joyce Chagonja akizungumza wakati wa mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na Viongozi wa Stand United

Mwenyekiti wa Stand United ya Mkoa wa Shinyanga inayoshiriki Ligi ya Championship, Stivian Antidius (Wenger) akiishukuru Benki ya NBC kwa kuwapatia elimu ya fedha wachezaji na viongozi wa timu hiyo

Meneja Maendeleo ya Biashara Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Regan Daud akielezea huduma za Kibenki zinazolewa katika Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United

Afisa Biashara Wateja Wadogo na wa Kati Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Allen Myalla akielezea kuhusu Masuala ya Bima, Mikopo na Akaunti mbalimbali zinazopatikana katika Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United

Afisa Biashara Wateja wa Kati na Wakubwa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Carlos Kapinga akielezea kuhusu masuala ya Fedha wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United
Afisa Biashara Wateja wa Kati na Wakubwa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga, Carlos Kapinga akielezea kuhusu masuala ya Fedha na Mikopo inayotolewa na Benki ya NBC wakati wa Mafunzo ya Fedha kwa Wachezaji na viongozi wa Stand United

Mmoja wa wachezaji wa Stand United akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo

Wachezaji wa Stand United wakiwa katika benki ya NBC Tawi la Shinyanga

Mkuu wa Kitengo cha Michezo Jambo Fm, Chris Kakwaya akifuatilia matukio wakati wa mafunzo hayo 
Viongozi wa Stand United wakiwa kwenye mafunzo hayo
Viongozi na wachezaji wa Stand United wakiwa kwenye mafunzo hayo

Picha ya kumbukumbu viongozi wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga na Viongozi , wachezaji wa Timu ya Stand United 

Picha ya kumbukumbu viongozi wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga na Viongozi , wachezaji wa Timu ya Stand United.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com