Na Sumai Salum _Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Modest Mkude amewataka watendaji na viongozi mbalimbali wilayani humo kutumia matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kama dira ya kutoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi.
Mkude ameyasema hayo leo Februari 13,2024 alipokuwa mgeni rasmi kwenye mafunzo ya siku moja ya usambazaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi kwa viongozi na makundi mbalimbali yaliyofanyika katika ukumbi wa Stage II hotel wilayani humo.
Amesema mafunzo hayo yaliyolenga kuwaongezea ufahamu na maarifa mazuri hasa viongozi na watendaji katika utungaji wa sera kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi kwenye eneo husika hivyo kutokana na dhamira njema ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan matokeo hayo yawe chachu ya mabadiliko chanya.
"Ni kweli dhima ya Rais wetu ni kuhakikisha haya matokeo ya sensa yanatusaidia na kuturahisishia kazi sisi watendaji kwani ofsi ya taifa takwimu imefanya kazi kubwa ya kukusanya taarifa za watu na makazi hivyo wananchi wanayo matumaini makubwa kuwa baada ya zoezi hili kukamilika kutakuwepo na mabadiliko chanya kwenye masuala ya maendeleo", ameongeza Mkude.
Aidha akiwasilisha maelezo ya mtakwimu mkuu wa serikali Bw. Benedict Mugambi ambaye ni meneja idara ya mifumo ya takwimu za kijiographia amesema awamu hii ya tatu(3) na ya mwisho ya usambazaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yanatakiwa yatumiwe na watunga sera nchini kwani yatasaidia kwenye mipango shirikishi kwa maendeleo endelevu.
Sambamba na hayo mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu na diwani wa kata ya Mondo mhe. Willium Jijimya ametoa rai kwa washiriki wote wa mafunzo hayo kuwa ni wawakilishi wa kundi kubwa la watu wanaowaongoza licha ya serikali kutumia gharama kubwa kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa wanapaswa kuinua na kuitekeleza miradi kwa kufuata takwimu hizo huku akiongeza kwa kuwataka madiwani watoe mapendekezo kwa Mkurugenzi wakati wa bajeti ili utengwaji mafungu uzingatie idadi ya watu.
Mbali na hayo matokeo ya sensa ya watu na makazi 2022 yanaonyesha hali ya wategemezi Tanzania bara kuwa 43% ya watu wote waliohesabiwa huku wilaya ya Kishapu kuwa ya pili katika mkoa wa Shinyanga kwa kuwa na wategemezi wengi ambapo kati ya watu 100 wenye nguvu za kufanya kazi wanategemewa na watu 106 ikiwa ni pamoja na kundi la watoto chini ya miaka 0-14 na wazee kuanzia miaka 65 na kuendelea ambapo kata ya Songwa ikiongoza kuwa na idadi kubwa ya wazee sawa na 7.0 ya watu wote waliohesabiwa huku Ushetu ikiwa ni ya kwanza kwa wategemezi wengi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye mafunzo ya usambazaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi yaliyofanyika siku moja Februari,13,2024 katika ukumbi wa Stage II hotel wilayani Kishapu.
Dkt. Mwinyi Omary Mwinyi kutoka ofisi ya taifa ya takwimu akitoa wasilisho la matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 katika mafunzo ya siku moja ya usambazaji wa matumizi yamatokeo ya sensa yaliyofanyika katika ukumbi wa stage ii hotel wilayani Kishapu.
Mwakilishi wa mtakwimu mkuu wa serikali ambae ni meneja idara ya mifumo na takwimu za kijiographia Bw.Benedict Mugambi akizungumzia awamu ya tatu ya matokea ya sensa ya watu na makazi 2022 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Stage II hotel iliyoko wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Madiwani wa kata za Kishapu mkoani Shinyanga wakifuatilia mafunzo ya usambazaji wa mtumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 yaliyofanyika ukumbi wa Stage II hoteli wilayani humo leo Februari 13,2024.
Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude akikabidhi ramani za matokeo ya sensa ya watu na makazi 2022 .
Viongozi wa kamati ya amani na maridhiano pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya usambazaji wa matumizi ya mtokea ya sebsa ya watu na makazi 2022 yaliyofanyika katika ukumbi wa Stage II hotel wilayani humo
Social Plugin