Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA AUAWA AKIAMUA UGOMVI WA MAMA MKWE AKIGOMBANIA MUME NA MWANAMKE MWENZAKE


Jaribio la mwanaume wa makamo kurejesha amani kati ya wanawake wawili wanaopigana limeisha kwa msiba eneo la Kericho nchini Kenya.

Mwanaume huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu na mwanamke aliyekuwa na hasira katika eneo la Kaplemeiwet huko Kipkoiyan kwenye pembetatu inayoshukiwa kuwa ya mapenzi.

Ripoti ya Citizen Digital ilisema mwanaume huyo aliingilia kati ili kusitisha vita kati ya mama mkwe wake na mwanamke mwingine. 

Mwanaume aliyekuwa akiishi eneo moja na mama mkwe wake alitahadharishwa na kelele nje na kukimbilia kuchunguza kilichokuwa kikiendelea.

Mwanaume wa Kericho alidungwa vipi 

Alipofika nje, inasemekana alimkuta mama mkwe wake akipigana na mwanamke mwingine anayeishi katika eneo moja.

Kulingana na wenyeji, wawili hao walikuwa wakipigana kuhusu mwanamume ambaye alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mvamizi huyo.

Hata hivyo, walidai kuwa kulikuwa na minong’ono kwamba mwanamke mwingine pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi sawa na huo. 

Mabishano yalizuka kati ya wawili hao, na kuzidi kuwa makabiliano ya kimwili.

Marehemu aliingilia kati na kujaribu kuwatenganisha wawili hao kwa kumvuta mama mkwe wake kando.

Kabla hajamvuta kabisa yule mwanamke mwingine akatoa kisu cha jikoni akikusudia kumchoma mpinzani wake na kumlenga lakini kikapenya shingoni mwa mwanaume huyo na kumuua.

Kwa nini mwanaume huyo wa Kericho hakuokolewa?

 Walioshuhudia vita hivyo walibaini mtu huyo amechomwa kisu na kusogea kumwokoa, lakini alifariki dunia wakati akikimbizwa hospitali.

Kwa kutambua alichofanya, bibi huyo anadaiwa kutumia fursa ya kuchanganyikiwa kutoroka eneo la tukio. 

Waliripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Sosiot, ambapo maafisa walijibu na kuhamisha mwili huo hadi katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Kericho. 

Maafisa wameendelea kuzunguka eneo hilo huku msako wa kumtafuta bibi huyo ukizidi.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com