Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NJIA ZA KUZUIA MATUMIZI MABAYA YA SIMU, TV NA LAPTOP

Kuweka simu yako mbali na chumba chako cha kulala husaidia kupata usingizi mzuri usiku.

Maelezo kuhusu taarifa Author,Paul Levy

Utafiti unaonesha kuwa mtu wa kawaida hutumia takribani saa saba kwa siku kwenye intaneti. Na saa hizi huwa nyingi zaidi ikiwa unafanya kazi inayokuhitaji kutumia kompyuta.

Wengi wetu hutumia vifaa vya kidigitali kupita kiasi na hutumia muda mwingi kufanya kazi au kuchezea simu za mkononi, vishikwambi na kompyuta.

Kuna utegemezi mkubwa wa teknolojia na kuna onyo kuhusu hatari kwa afya yetu ya kimwili na kiakili.

Mara nyingi binadamu hukimbilia katika ulimwengu wa kidigitali ili kuepuka msongo wa wazo wa ulimwengu wa kimwili. Lakini tunaishia kukusanya aina nyingine ya msongo wa mawazo.


Ni vigumu kupuuza ukweli kwamba teknolojia nyingi zinaweza kusababisha matatizo kwa sisi wanadamu.


Ni muhimu kuelewa kwamba vifaa vya kidigitali vina faida kama vile kupata marafiki, elimu na burudani. Hatari hutokea wakati wa matumizi ya kupita kiasi.


Jinsi ya kudhibiti matumizi mabaya ya vifaa vya teknolojia.

Jizoeshe kukaa mbali navyo

Usiache vifaa vyako vionekane machoni na kuviweka karibu yako wakati huvitumii, hasa usiku. Ondoa vifaa hivyo kwenye chumba chako cha kulala.


Acha tabia ya kutazama TV ukiwa na simu yako karibu nawe. Zingatia kazi moja kwa wakati mmoja, bila ya kuendeshwa na vifaa vingi.

Weka ukomo wa muda

Kutumia muda mwingi ukiwa na kifaa cha teknolojia kunaweza kusababisha maumivu ya kichwa.


Tumia teknolojia kwa uangalifu. Nunua saa ya kengele na usitumie kengele ya simu yako ya mkononi.


Tumia programu za kufuatilia muda hupima muda gani unaotumia (kupoteza) kutazama simu.

Zuia usumbufu

Kutumia saa ya mkononi huondoa hitaji la kuchukua simu yako ili kuweka kengele.

Usumbufu wa mara kwa mara unaweza kusababisha msongo wa mawazo na uchovu wa mwili.

Zima jumbe za arifa unapotaka kufanya jambo fulani. Na usiache simu yako ya mkononi kwenye dawati lako.

Utafiti unaonesha kuweka simu ya mkononi karibu, hata ikiwa hailii au haitetemeki (na hata kama kifaa kimezimwa), kunaweza kutatiza utendaji kazi.

Jiondoe katika mazingira ya kidigitali

Kutumia sana intaneti ni sababu ya unyongovu na wasiwasi. Unapaswa kujiweka mbali na ulimwengu wa kidigitali kwa muda.

Nenda matembezi, soma kitabu, endesha baiskeli, fanya shughuli yoyote ambayo inakuondoa kwenye simu, tv au kompyuta kwa muda.

Punguza mwanga

Utumiaji mwingi wa simu, tv au kompyuta unaweza kuharibu macho yako na kuharibu uwezo wako wa kuona.

Punguza mwanga wa vifaa vyako na anza kwa kudhibiti mwanga wa simu na uhakikishe sauti ya simu sio kubwa.
Je, unaweza kusoma kitabu kwa muda gani bila kuangalia simu yako ya mkononi?

Kaa mkao sahihi

Tumia mkao ambao hautadhuru shingo na mgongo wako.

Simama wima, nyoosha mwili mara kwa mara na fanya mazoezi mara kwa mara.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com