Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAAFISA KILIMO NA WATENDAJI KATA WAAGIZWA KUSIMAMIA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Kisena Mabuba amewaagiza Maafisa Kilimo na Watendaji wa Kata kuhakikisha wanadhibiti utoroshaji wa mazao na kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani  kwa kuwa dhamira ya Serikali ni kuona sekta ya kilimo inawanufaisha wakulima  na Serikali inapata ushuru. 

Hayo ameyasema leo Februari 19, 2023 katika kikao baina yake na Maafisa Kilimo, Maafisa Mifugo na Watendaji wa Kata  kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri . Kikao kazi hicho kililenga  kujadili utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mazao ya choroko na dengu.

“Kwetu sisi mfumo wa stakabadhi ghalani utatusaidia sana katika ukusanyaji wa mapato, hatutakuwa na kukimbizana na malori yanayotoroka kwa sababu wakiuza na wakinunua mazao ,hela yetu inaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya halmashauri”alisisitiza.


Katika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani unaanza mara moja,  Bw. Mabuba amewaagiza Mkuu wa Division ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na  Afisa Ushirika kupitia vyama vya msingi vya ushirika (AMCOs) na maghala  yote ya kukusanyia mazao yaliyopo katika Halmashauri na kubaini changamoto zilizopo ili ziweze kutatuliwa haraka.

Matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani  ni utekelezaji wa agizo la Serikali na maazimio ya wadau wa mazao ya mikunde katika mkoa wa Shinyanga waliokubaliana  kwa pamoja Februari 15,2025  kuwa mazao ya choroko na dengu yauzwe kwa  mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumwinua  mkulima kiuchumi.  Mfumo huo utawezesha wakulima wa mazao ya choroko na dengu kuwa na uhakika wa soko na kuuza mazao yao kwa bei yenye faida  na kuinuka kiuchumi pamoja na kuongeza uzalizaji wa mazao kwa tija na ubora zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com