EWURA KUBORESHA UANDAAJI MPANGO WA BIASHARA KWA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI


Kaimu Mkurugenzi Mkuu EWURA, Mha. Poline Msuya, akitoa neno la ufunguzi katika Mkutano huo.
Baadhi ya Wadau kutoka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Poline Msuya (aliye keti katikati) katika picha ya Pamoja na Menejimenti ya EWURA na baadhi ya Wadau kutoka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini, mara baada ya kufungua mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imekutana na wadau kutoka Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira nchini (WSSA) ili kujadili na kuboresha Muundo mpya wa Mpango wa Biashara kwa Mamlaka za maji nchini ili kuongeza ufanisi katika uandaaji wa mipango hiyo na kutoa huduma bora, leo tar.15/02/2024, Dodoma.

Akifungua mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Poline Msuya alisema, “EWURA imebaini kuwa, mipango mingi ya biashara kutoka WSSAs imekuwa na changamoto ya kutofautiana kwa takwimu na taarifa, jambo linaloleta ugumu katika mapitio ya mipango hiyo na upangaji wa bei”

“Ili kukabiliana na changamoto hiyo, EWURA imeandaa Muundo wa Mpango wa Biashara ili kurahisisha maandalizi ya mpango wa biashara kwa WSSAs na kuendana na Muongozo ya Upangaji Biashara, 2022” aliongeza.

Akitoa maoni yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Igunga, Mha. Humphrey Mwiyombela, ameipongeza EWURA kwa kuandaa muundo utakao warahisishia uandaaji wa mpango wa biashara na kuiomba EWURA kuongeza sehemu ya ufuatiliaji na tathimini ya taarifa wanazoziweka ili kuwasaidia kuona mapungufu katika taarifa zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post