Mhandisi Mwandamizi wa Umeme, EWURA Kanda ya Kati, akiwaonesha wanafunzi wa VETA Iringa, madaraja ya leseni za umeme zinazotolewa na EWURA kwa mafundi umeme nchini, wakati wa mafunzo ya EWURA kwa wanafunzi hao
Wanafunzi wa VETA Iringa wakifuatilia mafunzo yaliyotolewa na EWURA Chuoni hapo.
Wanafunzi wa VETA Iringa wakinyoosha mikono kuuliza maswali wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika chuoni hapo.
Na.Mwandishi Wetu_IRINGA
Mhandisi Mwandamizi wa Umeme wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Nicholaus Kayombo amesema EWURA sasa imerahisisha utoaji leseni za usanikishaji mifumo ya umeme kwa kuboresha mfumo wake wa LOIS unaotoa huduma za leseni kwa njia ya kieletroni.
Mha. Kayombo alieleza hayo, Jumatano, tar 31. 01.2024, wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wanaosomea usanikishaji mifumo ya umeme katika Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi -VETA Iringa, ambapo aliwasisitiza kupata leseni hizo kutoka EWURA pindi wanapomaliza masomo yao ili kukidhi matakwa ya Sheria, usalama na ubora wa huduma.
Alisema kutokana na mahitaji ya leseni hizo kuongezeka, EWURA imeboresha zaidi huduma zake kidijitali na sasa mtu yeyote mwenye elimu ya umeme anaweza kufanya maombi, malipo na kupokea leseni kiganjani mwake kupitia barua pepe yake bila kulazimika kufika ofisini.
“ Mfumo wa LOIS unapatikana kwenye tovuti kupitia www. ewura.go.tz; na ni rahisi kuutumia, ingia, jisajili, omba na pokea leseni,”alisema.
Afisa Huduma kwa Wateja EWURA Kanda ya Kati, Bw. Juma Singano, aliwaeleza wanafunzi hao kuwa EWURA inao utaratibu mzuri wa kupokea na kushughulikia malalamiko yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa, hivyo wanapokuwa na malalamiko wayawasilishe ili kupata suluhu.
Mratibu wa Mafunzo VETA Iringa, Bw. Edmund Enugu litoa shukrani kwa EWURA na kuomba mafunzo ya aina hiyo kuwa endelevu.
Social Plugin