JESHI la
Polisi mkoani Shinyanga, limepanda miti katika maeneo ya Kambi na maeneo ya makazi ya Askari polisi wa Jeshi hilo ili kuboresha mazingira pamoja na
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Zoezi hilo la upandaji miti
limefanyika leo Febuari 14, 2024 ambapo miti 1600 imepandwa katika maeneo ya kambi
ya Jeshi la Polisi (FFU) na eneo la makazi ya Askari polisi uwanja wa polisi
Kambarage .
Akizungumza wakati wa kupanda miti,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Jeshi hilo
linaunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kampeni ya
upandaji miti ili kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi.
“Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga tumepanda
Miti 1600, lengo ni kuunga mkono juhudi za viongozi wetu katika kampeni ya
upandaji miti kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,”amesema
Magomi.
“Katika kampeni ya upandaji miti
tunataka Shinyanga iwe ya kijani, na miti ambayo tunaipanda tunataka ilindwe na
ikue, ,”ameongeza Magomi.
Askari Polisi mkoa wa Shinyanga wakionyesha utayari wa kupanda miti katika maeneo ya makazi yao
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akimfundisha uzalendo mtoto juu ya utunzaji wa mazingira
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Janeth Magomi akimfundisha uzalendo mtoto juu ya utunzaji wa mazingira