Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Ameir (MgeniRasmi) akitoa nasaha zake kwa wahitimu wa Mpango wa Ufadhili kwa Vijana kutoka Kaya Maskini na wanaoishi katika mazingira magumu waliofadhiliwa na Mamlaka ya Elinu Tanzania. Hafla hiyo ya mahafali imefanyika jana Mkokotoni, Unguja.
*****************
Na Mwandishi wetu
MNAMO Desemba 14, 2022, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilizidua rasmi Mpango wa Ufadhili waMafunzo ya Ujuzi kwa Vijana wanaotoka Kaya Maskini na Wanaoishi katika Mazingira Magumu kwa upande wa Zanzibar.
Mafunzo hayo yalikuwa ya muda mfupi kati yawiki mbili hadi miezi mitatu na yalilenga kuwanufaishavijana wanaotoka katika kaya maskini waliosajiliwakatika Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliwaweze kujikomboa kiuchumi.
Mpango huo umetekelezwa kwa mafanikio makubwasana ambapo jumla ya vijana 600 wamefanikiwa kupatamafunzo ya ujuzi katika fani mbalimali kama vile mapishi, ushoni, ufundi magari, ufundi umeme, kilimocha mbogamboga, uchomeleaji wa vyuma pamoja naufundi bomba. Kati ya wanufaika hao 600, jumla yawanufaika 300 wametoka katika kisiwa cha Unguja na300 wametoka Pemba.
Akizungumza jana januari 31 Kaskazini Unguja katikahafla ya kuwapongeza na kuwatunukia vyeti wanufaikahao Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo yaAmali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Ameir amesema, niwakati muafaka sasa kwa wanufaika hao kwendamtaani kuzitafuta fursa kwani tayari wana ujuzi na vyetiwanavyo.
‘‘Ni wakati wa kwenda kujichangaya mtaani sasa ili fursaziwaone maana fursa zipo kila mahali ila sharti ni lazimautoke hapo ulipo, ufanye kitu hata kama kitakuwahakikulipi kwa wakati huo ili ujuzi ulio nao uonekane namwisho fursa zitakufuata, amesema Dkt. Mwanakhamis’’.
Aidha ameongeza kuwa, Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar, zinatambua uwepo wa kaya masikini katikajamii zetu na zinatambua uwepo wa changamoto nyingiambazo zinakabili familia hizo ikiwemo kipato cha chinikinachopelekea kiwango duni cha upatikanaji wahuduma za msingi.
Amesema, katika kukabilia na changamoto hiyo, Serikaliya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa Kushirikianana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia mradi waKuendeleza Ujuzi (SDF) iliona njia mbadala yakupunguza au kuondoa ugumu wa maisha kwa familiaza kaya maskini ni kuwapatia vijana wanaotoka katikafamilia hizo taaluma ya ufundi kupitia fani tofauti ilivijana hao waweze kujiajiri au kuajiriwa na kupata kipatokitakachosaidia familia zao.
‘‘Nafarijika sana kuwa hapa leo ili kuwapongeza nakuwatunukia vyeti vijana 600 ambao wamenufaika namafunzo ya ujuzi kupitia Mpango wa Ufadhili kwa Vijanakutoka kaya maskini. Mradi huu unaendana kabisa navipaombele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar vyakuandaa mageuzi katika sekta ya elimu kwa kuwekezakatika mafunzo ya amali, amesema Dkt. Mwanakhamis’’.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradiMkurugenzi Mtendaji, Mamlaka ya Mafunzo ya AmaliZanzibar. Dkt. Bakari Silima amesema, kwanza anaishukuru sana TEA kwa kuwakumbuka vijana kutokakaya maskini na kuwapa ufadhili wa huo wa mafunzo yaujuzi.
Amesema, kutokana na kipato duni walicho nacho vijana hao wengi wanakwama kuzifikia fursa hivyowamekuwa wakiwahimiza kujiunga katika vikundi iliwaweze kupata msaada kutoka kwa wadau, mashirika, taasisi na pia Serikali kupitia idara ya vyama vyamaushirika.
Nae mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya ElimuSayansi na Teknolojia Bw.Ephrahim Simbeye amesema,mwaka 2020/2021, Serikali ya jamhuri ya Muungano waTanzania na Benki ya Dunia zilikubaliana kuanzishaMpango wa Ufadhili wa Mafunzo ya Ujuzi kwa Vijanawanaotoka Kaya Maskini na Wanaoishi katika MazingiraMagumu (Bursary Scheme for Vulnerable Groups) uliowekwa kuwa sehemu ya ufadhili wa Mfuko waKuendeleza Ujuzi (SDF) chini ya usimamizi wa TEA.
Ameongeza kuwa, katika kukabiliana na changamoto yanguvu kazi isiyo na ujuzi wa kutosha unaotakiwa katikasoko la ajira, Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, zimewekamikakati mbalimbali inayolenga kuleta mageuzimakubwa ya kiuchumi.
Amesema mikakati hiyo inalenga kufikia lengo la nanela Umoja wa mataifa la Maendeleo Endelevulinaloazimia mataifa kuchangia ukuaji wa uchumiendelevu, ajira kamili zenye tija, na kazi zenye stahakwa wote, na kuwawezesha wananchi kupata Ujuzi nafursa za kiuchumi ili kupunguza umaskini wa kipato nakuongeza tija katika shughuli za kiuchumi.
Kwa upande wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi waMiradi Bw. Masozi Nyirenda amesema, lengo la Mpangolilikuwa kufadhili Mafunzo kwa Jumla ya Wanufaika4,000 nchi nzima, ambapo hadi sasa jumla ya vijana4,063 wameshanufaika, ikiwemo vijana 600 wa Zanzibar ambao wamekabidhiwa vyeti vyao.
Mpango Ufadhili wa Mafunzo ya Ujuzi kwa Vijanakutoka Makundi Maalumu na Wanaoishi katikaMazingira Magumu ni sehemu ya utekelezaji wa Mradiwa Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund -SDF) chini ya Programu ya Kukuza Ujuzi na Stadiza Kazi kwa ajili ya Ajira zenye Tija (Education and Skills for Productive Jobs-ESPJ) unaoratibiwa naWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mfuko wa SDF ulikuwa unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Benki ya Dunia.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Ephrahim Simbeye akitoa salamu kutoka kwa viongozi wa Wizara katika mahafali ya vijana kutoka kaya maskini waliosoma mafunzo ya amali kupitia ufadhili wa TEA.
Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali naUsimamizi wa Miradi kutoka TEA Bw. Masozi Nyirenda akielezea kuhusu Mpango wa Ufadhili kwa Vijana kutoka Kaya Maskini na wanaoishi katika mazingira magumu katika mahafali ya vijana hao yaliyofanyika Unguja Zanzibar
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Ephrahim Simbeye akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi kutoka TEA Bw. Masozi wakati wa mahafali ya vijana kutoka kaya maskini yaliyofanyika Unguja Zanzibar
Mgeni Rasmi Dkt. Mwanakhamis Ameir akitoa cheti kwa mmoja wa wanufaika wa Mpango wa Ufadhili kutoka Kaya Maskini waliosoma mafunzo ya amali kupitia ufadhili wa TEA.
Mgeni Rasmi Dkt. Mwanakhamis Ameir akitoa cheti kwa mmoja wa wanufaika wa Mpango wa Ufadhili kutoka Kaya Maskini waliosoma mafunzo ya amalikupitia ufadhili wa TEA. Kulia kwake ni Bw. Ephrahim Simbeye, mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Masozi Nyirenda Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi kutokaTEA. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji, Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar. Dkt. Bakari Silima.
Sehemu ya wanufaika wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali ya vijana kutokakaya maskini yaliyofanyika Unguja Zanzibar
Baadhi ya wanufaika wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Dkt. Mwanakhamis Ameir mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao.
Mkurugenzi Mtendaji, Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar. Dkt. Bakari Silima akitoa taarifa jinsi mafunzo yalivyotekelezwa kwa vijana kutoka kaya maskini waliosoma mafunzo ya amali kupitia ufadhili wa TEA
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo yaAmali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Ameir (MgeniRasmi) akiteta jambo na Bw. Ephrahim Simbeyemwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakati wa mahafali ya vijanakutoka kaya maskini yaliyofanyika Unguja Zanzibar.
Social Plugin