MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Fadhili Maganya,akizungumza wakati wa kikao cha kutambulisha kamati ndogo ndogo tano za kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja huo uliofanyika leo Februari 21,2024 jijini Dodoma.
MAKAMU Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bi. Dogo Iddi Mabrouk,akizungumza wakati wa kikao cha kamati ndogo ndogo tano za kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja huo kilichofanyika leo Februari 21,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya Wajumbe wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw. Fadhili Maganya (hayupo pichani),akizungumza wakati wa kikao cha kutambulisha kamati ndogo ndogo tano za kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja huo kilichofanyika leo Februari 21,2024 jijini Dodoma.
MJUMBE wa Kamati ya maadili na elimu aliyepewa jukumu la kusimamia mapitio ya shule hizo, Kanali Mstaafu, Iddy Kipingu,akizungumza wakati wa kikao cha kamati ndogo ndogo tano za kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja huo kilichofanyika leo Februari 21,2024 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM),imeonya kwa baadhi ya vyama vya upinzani vinavyobeza jitihada zinazofanywa na Rais Dkt . Samia Suluhu Hassan, kumuacha aendelee kufanya ziara nje na ndani ya nchi ili kutafuta fursa za kuifungua nchi.
Onyo hilo limetolewa leo Februari 21,2024 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Fadhili Maganya wakati wa kikao cha kutambulisha kamati ndogo ndogo tano za kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja huo.
“ Nchi hii si iliyoendelea bali inaendelea, ni kweli tuna uhuru lakini hatuwezi kupiga hatua haraka tunaenda taratibu, mwenda bure si sawa na mkaa bure huenda akaokota, mgaa gaa na upwa hali wali mkavu pia mguu mtembezi usiporudi na umande utarudi na mwiba.”
“Niwaombe na kuwasihi ndugu zetu wa vyama vya upinzani,tumuache Rais Samia aendelee na ziara za ndani nan je ya nchi ili aifungue nchi, niwaonye wote wanaobeza jitihada anazofanya Rais, wamuache,”.amesema Mwenyekiti Maganya.
Mwenyekiti Maganya ametumia fursa hiyo kueleza dhamira ya kuzibadilisha baadhi ya shule zinazomilikiwa na jumuiya hiyo ili ziingie kwenye mfumo wa vyuo vya kati.
“Katika uboreshaji wa shule zetu kupitia mwongozo ulioridhiwa na Baraza la wadhamini wa CCM, tumeruhusiwa kuingia ubia au kukaribisha wabia na wawekezaji mbalimbali bila ya mipaka kuungana nasi katika kuendesha hizi shule,hivyo tumepokea ombi umepokea ombi kwamba baadhi ya shule tunazibadili na kuzipeleka katika mfumo wa vyuo vya kati,na huo ulikuwa ndio utashi wetu,
Awali,Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Dogo Iddi Mabrouk amesema jumuiya hiyo ni kubwa haina ubaguzi inachukua watu wa rika zote hivyo itandelea kusimamia suala la maadili.
“Nawapongeza wote mliopata uteuzi huu kwenye kamati na hiyo ndio lengo la kujenga jumuiya yetu tukiamini kwamba tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha jumuiya yetu inasonga mbele na kuwa mfano ndani ya Chama cha Mapinduzi,kwa hili sina wasiwasi ,”amesema.
Nae,Mjumbe wa Kamati ya maadili na elimu aliyepewa jukumu la kusimamia mapitio ya shule hizo, Kanali Mstaafu, Iddy Kipingu ameeleza dhamira ya jumuiya ya kusimamia shule inazoziendesha.
“Turudi nyuma shule zetu za wazazi,wazazi sisi ndio walezi ,tunazungumza kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo,aanze kutengenezwa akiwa mchanga,sasa yale tunayoyazungumza tuyatekeleze kwa vitendo,”amesema.
Kamati ndogo ndogo tano zilizoundwa ni kamati ya fedha,uchumi ,mipango na uwekezaji,kamati ya afya na mazingira,kamati ya elimu na malezi ,kamati ya michezo,utamaduni na sanaa na kanuni,maadili na sheria.
Social Plugin