MTATURU ALIA NA SEKTA YA MAZIWA



 Mbunge wa Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu,akiuliza swali bungeni jijini Dodoma .

.........

SERIKALI imemhakikishia mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu kuwa itaenda kuweka vituo vya kukusanyia maziwa na vifaa vya kutunzia maziwa katika Mkoa wa Singida ili yasiharibike na hivyo kuvutia wawekezaji.



Kauli hiyo ya serikali inajibu swali lililoulizwa na Mbunge Mtaturu ,Bungeni Jijini Dodoma.

“Ili serikali iweze kuweka uvutiaji wa wawekezaji katika sekta ya maziwa ni wajibu wake pia kujenga vituo vya kukusanyia maziwa,Je ni nini mpango wa serikali wa kuweka vituo vya kukusanyia maziwa katika Mkoa wa Singida ili kuwavutia wawekezaji katika eneo hilo,”amehoji Mtaturu.

Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji,Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Excaud Kigahe amesema moja ya maeneo ambayo serikali ya awamu ya sita inaweka msisitizo sana ni maeneo ya vituo vya kukusanya maziwa na hasa kuweka vifaa vya kuhifadhia maziwa hayo.

“Vifaa hivyo vitasaidia kutunza maziwa,kwa hiyo nimhakikishie mbunge Mtaturu kwamba eneo hili pia tutakuja kuweka vituo hivyo vya kukusanyia maziwa na hasa vifaa hivi vya kutunzia maziwa ili yasiharibike wakati yanasubiri kwenda kwenye viwanda,”.amesema Naibu Waziri huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post