Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATAKA WATUMISHI WA AFYA SHINYANGA KUZINGATIA MAADILI.. AONYA KUTOA SIRI ZA WAGONJWA

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza katika Jengo Jipya la Wagonjwa wa Dharura Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,amefanya ziara mkoani Shinyanga na kutoa Maagizo kwa Watumishi wa Afya kutoa huduma stahiki za matibabu kwa wagonjwa.
Amefanya ziara hiyo leo Februari 23,2024, kwa kuona utoaji wa huduma za Afya katika Kituo cha Afya Kambarage, huduma katika jengo la wagonjwa wa dharura na Ujenzi wa OPD Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na huduma za matibabu hospitali ya Rufaa Mkoa pamoja na kuzungumza na Watumishi wa Afya.

Amesema Serikali imeboresha utoaji wa huduma za Matibabu kwa wananchi,kwa kujenga Zahanati,Vituo vya Afya, hospitali pamoja na kutoa vifaa tiba vya kisasa, na hivyo kuwataka Watumishi wa Afya kutoa huduma stahiki za matibabu kwa wagonjwa.
Amesema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Serikali itaongeza pia ujenzi wa Majengo matano ili kuboresha huduma za Matibabu, ikiwamo ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto,Maabara, Stoo ya dawa, Mochwari na Jengo la kufua nguo za Wagonjwa.

"Tunataka Maboresho haya ya huduma za Afya, yaendane na utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wananchi," amesema Dkt. Magembe.
Katika hatua nyingine ametoa Maagizo kwa Watumishi wa Afya, kuzingatia Miiko,Sheria,kanuni na maadili ya taaluma zao pamoja na kutunza siri za Wagonjwa.

Amesema kwa Mtumishi wa Afya ambaye anakwenda kinyume na Maadili ya Taaluma yake na kuitia doa Sekta hiyo, hawata sita kumchukulia hatua kwa kumuondoa kazini na hata kufutiwa leseni yake.
Pia ameagiza ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga,kwamba ukamilike kwa wakati ili lianze kutumika kutoa huduma kwa wananchi, ambalo linatarajiwa kukamilika Machi mwaka huu.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile, ameipongeza Serikali kwa kuboresha huduma za Afya mkoani humo,na kwamba baadhi ya huduma ambazo Wananchi walikuwa wakienda kupata Bugando Jijijini Mwanza,sasa hivi zinapatikana mkoani humo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, amesema maelekezo yote ambayo yametolewa watayafanyia kazi, ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na Watumishi wa Afya wa Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiendelea kuzungumza na Watumishi wa Afya mkoani Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wagonjwa katika Kituo cha Afya Kambarage.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, akiangalia Kifaa Tiba cha Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Kambarage ambacho kitafanya uchunguzi wa Meno na kutoa Tiba na siyo kung'oa meno tena.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiangalia uandikishaji wa Wagonjwa kwa mfumo wa Mtandao katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiendelea kukagua ubora wa utoaji huduma katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akifuatilia huduma za mapokezi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akiangalia namna uzalishaji wa Hewa ya Oxgyen katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe akizungumza na wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Watumishi wa Afya wakiwa kwenye kikao cha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe wakisikiliza maelekezo ya Serikali juu ya utoaji wa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com