Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RUFAA YA MARIA NGODA ALIYEFUNGWA MIAKA 22 KWA KUKUTWA NA NYAMA YA SWALA YASIKILIZWA


Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu ya Mkoa wa Iringa chini ya Jaji Mfawidhi Mgetta leo Februari 1, 2024 imesikiliza kesi ya Rufaa Namba 84101/2023 kati ya Maria Ngoda dhidi ya Jamuhuri.

Akiongoza jopo la Mawakili upande wa mkata rufaa Wakili Moses Ambwindile amesema leo wametetea sababu zao za Rufaa 14 mbele ya Jaji Mfawidhi.

Aidha Jaji Mgetta ameahirisha shauri mpaka hapo kesho tarehe 2 Februari 2024. Mfungwa Maria Ngoda (mkata rufaa) alihukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala Novemba 3 Novemba 2023

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com