TBS YAWATAKA WAZALISHAJI WA BIDHAA ZA UNGA NA SIAGI ZA KARANGA KUZALISHA BIDHAA ZINAZOKIDHI VIWANGO

Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akifungua kikao cha wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini kilichofanyika leo Februari 14, 2024 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam

**********


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limewataka wazalishaji, waingizaji na wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini kuzalisha, kuingiza na kusambaza bidhaa zilizokidhi viwango ili kulinda afya ya mlaji pamoja na masoko ya ndani na nje ya nchi.


Akizungumza wakati akifungua kikao cha wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema kuwa TBS inawajibika kikamilifu kuhakikisha kuwa chakula pamoja na bidhaa nyingine zinazozalishwa hapa nchini na zile zinazotoka nje ya nchi zinakidhi matakwa ya viwango kwa lengo la kulinda afya ya jamii, kuwezesha biashara na kukuza uchumi wa nchi.

"Sote tunatambua kuwa bidhaa zitokanazo na nafaka hususan unga pamoja na bidhaa za karanga ni mojawapo ya vyakula vinavyotumika kwa wingi hapa nchini; hivyo basi, endapo bidhaa hizo hazitakidhi matakwa ya usalama na ubora huweza kusababisha madhara ya kiafya na kiuchumi". Amesema

Aidha amesema kuwa, TBS itaendelea kutilia mkazo suala la usimamizi wa viwango na kudhibiti usalama na ubora wa bidhaa hizo pamoja na aina nyingine za bidhaa za chakula.

Pamoja na hayo amesema kuwa wanatambua umuhimu wa bidhaa zitokanazo na nafaka hususan unga wa mahindi na nafaka nyinginezo pamoja na bidhaa zitokanazo na karanga.

Amesema kuwa Chakula kisipokuwa salama husababisha madhara ya kiafya na hata vifo kwa walaji sanjari na athari za kiuchumi. Hivyo ikumbukwe kuwa chakula kisipokuwa salama, hicho siyo chakula.

Kwa upande wake Mshiriki wa kikao hicho ambaye ni mzalishaji wa siagi za karanga nchini, Bi Janeth Mashauri amesema kuwa kukutana mara kwa mara na TBS inawasaidia kutengeneza bidhaa kwa kiwango cha hali ya juu ili kuepukana na madhara yatokanayo na sumukuvu na pia inawapa ujasiri katika uzalishaji wa bidhaa ambazo wanazizalisha nchini.

Amesema anawashauri wajasiriamali wanaohusika na utengenezaji wa unga kujitahidi kuhudhulia katika semina ambazo zinakuwa zinatangazwa na TBS kwasababu zitawasaidia kuweza kufanya biashara zao kwa uhakika.

Nae Mzalishaji wa unga ambaye pia ameshiriki kikao hicho, Bw. Baraka Nyerenda amesema kuwa mafunzo ambayo wamekuwa wakiyapata kutoka TBS, yanawapa uelewa sehemu ambayo wanahitaji kuboresha ili kuweza kuzalisha chakula bora kwaajili ya walaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akifungua kikao cha wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini kilichofanyika leo Februari 14, 2024 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini kilichofanyika leo Februari 14, 2024 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Dkt. Candida Shirima akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini kilichofanyika leo Februari 14, 2024 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Kaimu Meneja wa Ukaguzi na Uzingatiaji wa Sheria (TBS) Bw. Moses Mbambe akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini kilichofanyika leo Februari 14, 2024 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wazalishaji, waingizaji na wasambazaji wa bidhaa za unga wa mahindi, unga mchanganyiiko na siagi ya karanga nchini wakiwa katika kikao na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kilichofanyika leo Februari 14, 2024 katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post