Meneja Rasilimaliwatu na Utalawa EWURA, Bw. George Seni ( kushoto) akiwaonesha watendaji wa Tume ya Udhibiti wa Huduma za Umma Ghana (PURC) mazingira ya ofisi ya EWURA makao makuu Dodoma, leo 28.02.2024
Na.Mwandishi Wetu_DODOMA
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imekutana na Menejimenti ya Tume ya Udhibiti wa Huduma za Umma Ghana (PURC) katika Ofisi za EWURA Makao makuu jijini Dodoma ili kuwapatia mafunzo kuhusu udhibiti.
Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mha. Gerald Maganga alisema “ EWURA inawakaribisha sana, na ipo tayari kuwapatia mafunzo mbalimbali ya udhibiti na hamtojutia ziara yenu ya mafunzo kuhusu udhibiti”.
Meneja Ufundi wa Maji na Usafi wa Mazingira EWURA Mha. Titus Safari alielezea kwa kina namna EWURA inavyodhibiti huduma, kazi pamoja na majukumu ya EWURA.
Mkurugenzi wa Huduma za Maji na Ufuatiliaji wa Utendaji kazi PURC Ghana, Mha. Emmanuel Fiati ameipongeza EWURA kwa mafunzo hayo na kueleza kwamba “ nimefurahia mafunzo haya na yamenivutia sana”
Mafunzo hayo ya siku nne yalianza tarehe 26 Februari 2024.
Meneja Ufundi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira EWURA Mha. Titus Safari (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Maji na Ufuatiliaji wa Utendaji kazi wa PURC Ghana Mha. Emmanuel Fiatti, muda mfupi baada ya mafunzo juu ya udhibiti yaliyotolewa na EWURA, kwa watendaji wa PURC ghana, jijini Dodoma leo tarehe 28.02.2024
Meneja Rasilimaliwatu na Utalawa EWURA, Bw. George Seni ( kushoto) akiwaonesha watendaji wa Tume ya Udhibiti wa Huduma za Umma Ghana (PURC) mazingira ya ofisi ya EWURA makao makuu Dodoma, leo 28.02.2024<
Social Plugin