Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DEREVA WA GARI LA WAGONJWA AFARIKI NA MGONJWA KWENYE AJALI

Watu wawili akiwemo mgonjwa aliyekuwa akipelekwa hospitali ya Rufaa Bombo na dereva wa gari la kubebea wagonjwa la Hospitali ya Magunga iliyopo Korogwe, wamefariki dunia, huku wengine wanne wakijeruhiwa, baada gari la wagonjwa walilokuwa wakilitumia, kugongana na Lori aina ya SCANIA, katika eneo la Chang'ombe, mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, ambaye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Lori ambaye alijaribu kuyapita magari mengine bila tahadhari na kwenye eneo ambalo haliruhusiwi.

Aidha, kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Magunga, Dr.Jery Kilwale, amesema wamepokea miili miwili pamoja na majeruhi wanne ambao waliwapa huduma ya kwanza na baadae walipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa ajili ya matibabu zaidi.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com