Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA SC YAICHAPA 4-0 CR BELOUIZDAD, YATINGA ROBO FAINALI CAFC


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali mara baada ya kufanikiwa kuinyuka CR Belouizdad kwa mabao 4-0 katika mchezo wa hatua ya Makundi Klabu Bingwa Afrika.

Yanga Sc ilikuwa inahitaji ushindi wa mabao 4-0 kwenye mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali kwani mechi ijayo ambayo Yanga Sc atacheza na Al Ahly hata kama akifungwa basi atakuwa amebaki na pointi 8 sawa na. Ambao nao wakishinda dhidi ya Medeama.

Katika mchezo huo ambao Yanga alikuwa mwenyeji na kuipa mechi hiyo PACOME DAY tumeshuhudia kandanda safi kupitia kwa Pacome na wachezaji wenzake na kufanikiwa kupata mtaji mkubwa wa mabao.

Mabao ya Yanga yamewekwa kimyani na Mudathir Yahya katika kipindi cha kwanza cha mchezo, mabao mengine yamefungwa na Aziz Ki, Kenned Musonda pamoja na Joseph Guede ambaye aliinhia kipindi cha pili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com