Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Watumishi kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) wametembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa namna ya upatikanaji maji chini ya ardhi.
Wageni hao wametembelea chanzo cha maji cha Nzuguni na kujionea kazi za uchimbaji wa visima zinazoendelea katika eneo hilo.
Jiji la Dodoma linahudumiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ambapo sehemu kubwa ya huduma ya maji inapatikana kutokana na visima kama ilivyo upande wa Zanzibar ambao pia sehemu kubwa ya huduma ya maji inapatikana kutokana na visima.
Social Plugin