Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MIRADI YA TACTIC KUNUFAISHA WANANCHI WA BAKOBA


Diwani wa kata ya Bakoba Shabani Rashid akiwahutubia wananchi wa kata hiyo

Na Mariam Kagenda - Bukoba
Diwani wa Kata ya Bakoba Shabani Rashid amesema kuwa ujio wa miradi mikubwa ya TACTIC katika Manispaa ya Bukoba  utawanufaisha kwa kiasi kikubwa wananchi wa kata ya Bakoba  kwani  zitajengwa Barabara za kisasa pamoja na ujenzi wa kingo za mto kanoni jambo ambalo litaondoa adha ya mafuriko kwa wananchi wa kata hiyo.

Mhe. Shabani amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Bakoba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 5 mwaka huu.

Amesema kuwa anaishukuru Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mikubwa ya  Elimu ,Afya pamoja na ujio wa Mradi mkubwa wa TACTIC ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa adha ya Barabara ambazo ni korofi katika kata ya Bakoba.

Katika kata hiyo barabara zitakazojengwa kupitia mradi wa TACTIC  ni pamoja na Barabara ya  Shaburdin-Buyekera, Buyekera-Nyakanyasi  na  Uhuru-Nyakanyasi hivyo kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa miundombinu hiyo ili kutimiza adhima ya serikali ya kutatua kero zinazowakabili wananchi 


Amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Adv. Stephen Byabato,Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatuma Mwassa , mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima, timu ya wataalamu Manispaa ya Bukoba,Tarura na waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya Bukoba wakiongozwa na Mstahiki Meya Gypson Godson  kwa namna wanavyoendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Manispaa hiyo.

Baadhi ya wananchi wa kata ya  Bakoba wamempongeza Diwani wao kwa jitihada kubwa za kuhakikisha kero zilizopo zinatatuliwa kwa wakati na kumuomba asikate tamaa na kuahidi kumpa ushirikiano mkubwa hasa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com