Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya Dhahabu ya Barrick ambayo inaendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals, kwa kufanya uwekezaji unaoendelea kuchangia kukuza uchumi na kufanikisha miradi ya kijamii ambayo inaendelea kuboresha maisha ya wananchi.
Mh. Mavunde ametoa pongezi hizo leo Jumatatu Machi 18,2024 wilayani Kahama wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa kijulikanacho kama Barrick Academy, katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama ambao umefungwa ambacho kitakuwa kinatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Barrick wa nchini na nje ya nchi kupata utaalamu wa kuendesha shughuli zao kwa weledi.
Waziri Mavunde amesema ulimwengu wa sasa ni wa sayansi na teknolojia hivyo chuo hicho kimeanzishwa katika wakati muafaka ambapo sekta ya madini nchini inakua kwa kasi sana na kuhitaji wataalamu wa kutosha.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) na Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde (kulia) wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick.
Ametoa wito kwa uongozi wa Barrick kuangalia uwezekano wa kuanzisha kozi za kuwasaidia wachimbaji wadogo wadogo nao wapate maarifa ya kuendesha kazi zao kwa maarifa.
“Barrick mmeanza kwa kufungua chuo katika eneo hili la Ukanda Maalum wa Kiuchumi la Buzwagi la Serikali, nina imani wawekezaji wengi watajitokeza kujenga viwanda ili kuziba athari za kiuchumi zilizotokana na kufungwa kwa mgodi wa Buzwagi”,amesisitiza.
Kwa upande wake, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, amesema Barrick itaendelea kufanya kazi na Serikali kuhakikisha ubia wake unanufaisha pande zote na kuchangia kukuza uchumi wa nchi.
Bristow amesema Barrick, inalipa umuhimu kubwa suala la elimu na itaendelea kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watanzania wanapata elimu na ndio maana imeamua kufungua chuo kikubwa cha kimataifa cha Barrick Academy nchini.
“Tutaendelea kuhakikisha kuwa ubia wetu na Serikali ya Tanzania unakuwa wa kuigwa katika sehemu mbalimbali duniani kwa kufanikisha kuleta mafanikio na maendeleo chanya kwa wananchi”, amesisitiza Bristow.
Bristow amesema Chuo cha Barrick kimebuniwa na Barrick ili kutoa programu maalumu za mafunzo zinazoandaliwa kulingana na mahitaji zinazolenga kuandaa mameneja wa mstari wa mbele wa Barrick ili wakue kama watu binafsi na viongozi katika nyanja zao huku kozi hizo zikiwapa ujuzi wa kusimamia timu zao kwa ufanisi zaidi na kuboresha utendaji.
“Chuo cha Barrick kitakuwa kikitoa mafunzo kwa mafomeni, wasimamizi na warakibu zaidi ya 2,000 kutoka Kannda ya Afrika Mashariki na Kati katika kipindi cha miezi 24 ijayo. Tukiwa na maono ya mbele, tunajitayarisha pia kuwajumuisha Wakandarasi wetu na kupanua mtaala ili kufikia taaluma nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na kutoa kozi za uongozi katika masuala ya fedha, ujuzi wa ngazi ya juu wa Kompyuta na katika masuala ya usalama”,ameongeza Bristow.
Ameeleza kuwa, ufunguzi wa chuo cha Barrick unafuatia ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Buzwagi Kahama mnamo mwezi Januari 2024 lililofungua fursa kwa ajili ya huduma za ndege zilizopangwa ambalo linaweza kuhudumia zaidi ya abiria 200 kwa wakati mmoja ambapo jengo hilo linatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji uchumi katika Manispaa ya Kahama.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Barrick katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Sebastiaan Bock amesema uwanja wa ndege na Chuo katika mgodi uliofungwa wa Buzwagi ni sehemu ya mpango wa Barrick wa kuibadili Buzwagi kuwa Ukanda Maalum wa kiuchumi.
“Upembuzi yakinifu uliofanyika mwaka 2021 ulionesha kuwa uundwaji wa Kanda maalumu ya kiuchumi ulikuwa na uwezo wa kuchukua nafasi ya mgodi wa Buzwagi kama kichocheo cha uchumi wa eneo hili na unaweza kutengeneza ajira zipatazo 3,000 kila mwaka, kuzalisha zaidi ya dola 150,000 kila mwaka kutokana na tozo za huduma kwa Manispaa ya Kahama na kutoa takribani dola milioni 4.5 kwa mwaka kama kodi ya ajira”,amesema Sebastiaan.
Amesema Serikali ya Tanzania iliidhinisha ubadilishaji wa mgodi wa Buzwagi kuwa ukanda maalum wa kiuchumi (SEZ) kupitia tangazo la Serikali ilitolewa mwezi Februari 2024 na tayari Wawekezaji wameanza mchakato wa kuanzisha viwanda katika eneo hilo.
“Namna tunavyofunga migodi yetu ni muhimu kwetu kama ambavyo tunaijenga na kuiendesha. Mgodi wetu wa Buzwagi ulikuwa kitovu cha uchumi katika ukanda huu kwa takribani miaka 15 kabla ya kutoa dhahabu yake ya mwisho mwaka 2021. Hata hivyo, mtazamo wetu huo siyo mwisho wa hadithi hii kwa Buzwagi tunapoibadilisha kuwa mali mbadala yenye tija ambayo itahudumia jamii kwa miongo kadhaa ijayo”,amesema Bock.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) Charles Itembe ameipongeza Kampuni ya Barrick kwa kubuni wazo la kuanzisha Chuo cha Barrick huku akiwaomba wawekezaji mbalimbali kujitokeza kuwekeza katika eneo hilo ili kuongeza thamani ya madini na vitu vingine kwenye eneo la Buzwagi ambako kutakuwa na viwanda zaidi ya 100 na mpaka sasa kuna wawekezaji wanane.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amesema kuanzishwa kwa Chuo cha Barrick ni matokeo mazuri ya ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick ili kukuza uwekezaji nchini.
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba amewapongeza Barrick kuwa wawekezaji wa kwanza katika Mgodi uliofungwa wa Barrick huku akiomba chuo hicho pia kitumike kutoa mafunzo ya madini kwa wachimbaji wadogo na jinsi ya kufanya biashara ya madini huku Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Thomas Muyonga akisema uwekezaji unaofanyika katika eneo hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kukuza uwekezaji nchini.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde akizungumza leo Jumatatu Machi 18,2024 wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick 'Barrick Academy' chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Barrick katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Sebastiaan Bock akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Barrick katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Sebastiaan Bock akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) na Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita (katikati) na Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick chenye hadhi ya kimataifa katika mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde (kulia) akiwa ndani ya moja ya madarasa katika Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde (katikati) akiwa ndani ya moja ya madarasa katika Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Muonekano ndani ya moja ya madarasa katika Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde (katikati) akiteta jambo na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (kushoto) katika Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Muokano sehemu ya majengo katika Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Muokano sehemu ya majengo katika Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Muokano sehemu ya majengo katika Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Meneja wa Barrick nchini, Melkiory Ngido akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama Mhe. Thomas Muyonga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) Charles Itembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde (kulia) wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick kwenye mgodi wa zamani wa Buzwagi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Barrick katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Sebastiaan Bock , kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde akiwa katika Chuo cha mafunzo cha Barrick
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick
Wadau wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde (katikati) akizungumza na viongozi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Chuo cha mafunzo cha Barrick
Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mavunde akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin