Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) leo Jumatatu Machi 25, 2024 limefanya uchaguzi mdogo kujaza nafasi zilizo wazi ndani ya Ofisi ambapo aliyekuwa Rais wa Bunge la Afrika PAP) Mhe. Chief Fortune Charumbira (Zimbabwe) amechaguliwa tena kuwa Rais wa Bunge la Afrika.
Katika uchaguzi huo pia Mhe. Prof. Massouda Mohamed Laghdaf (Mauritania) amechaguliwa tena kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika huku Mhe. Djidda Mamar Mahamat (Chad) akichaguliwa kuwa Makamu wa nne wa Rais wa Bunge la Afrika.
Social Plugin